Thursday, August 28, 2014

MISS SAN DIEGO KUPATIKANA JUMAPILI HII, TANDIKAKILE kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa San Diego Pub ‘Miss San Diego’ kinatarajiwa kufika kilele Jumapili hii, kwenye ukumbi wa Sun Diego, Tandika, jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Viumbe Wazito Promotion ambao ndio waandaaji wa kinyang’anyiro hicho wakishirikiana na San Diego Pub, Edson Ketto, ‘Mzee wa Channel Ten’ alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, jumla ya vimwana 10 watapanda jukwaani kuchuana siku hiyo.
Ketto alisema kuwa, kinyang’anyoro hicho kitapambwa na burudani kemkemu kutoka kwa wasanii wa Taarab na Bongofleva, wakiwamo Jokha Kassim, Dogo Mfaume, Inspekta Haroun na Ashura Machupa.
Ketto aliwaomba mashabiki pamoja na wapenzi wa tasnia ya urembo hapa nchini, kujitokeza kwa wingi, ili kushuhudia laivu kisura atakayetwaa taji hilo la Miss San Diego kwa mwaka huu.

UNAIJUA DOUBLE A MUSICA?


BENDI inayoongozwa na mkung’utaji tumba wa zamani wa Mlimani Park Sikinde, Abbas Abdallah, Double A Musica, jana alitimua vumbi zito la burudani, kwenye ukumbi wa Taxido, Buza Kanisani, jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari hizi alikuwapo ndani ya ukumbi huo wakati bendi hiyo ikifanya mambo yake na kushuhudia namna mashabiki walivyokuwa wakijimwaga katikati kwa wingi kucheza pamoja na kutuza baadhi ya wanamuziki walioonekana kuwavutia zaidi.
Mbali na kutumbuiza vibao vya kukopi, bendi hiyo pia ilipagawisha mashabiki kwa vibao vyao wenyewe ambavyo navyo vilionekana kukonga vilivyo nafsi za mashabiki waliokuwa wamehudhuria.

PATRICK KAMALEY ATUA EXCEL BAND

MKONGWE Patrick Kamalee akiwa na bendi yake mpya iitwayo Excel One, jana waliwasha moto mkali wa burudani katika kiwanja cha Kimboka Night Park, Buguruni, jijini Dar es Salaam na kukosha vilivyo nyoyo za mashabiki.
Kama kawaida, musicintanzania ilikuwapo eneo la tukio na kuwa shuhuda wa kile kilichokuwa kinaendelea ambacho si kingine bali ni burudani pevu kutoka kwa baadhi ya wanamuziki nguli wa miondoko ya dansi.
Bendi ya Excel inatumbuiza zaidi vibao vya kukopi kutoka kwenye bendi nyingine ambazo kwa sasa hazipo katika ulimwengu wa muziki, ambapo nyimbo nyingi ni kutoka kwenye makundi aliyowahi kuyatumikia Kamalee.


PATRICK KAMALEY
EXTRA BONGO NDANI YA UKUMBI WA FLAMINGO MAGOMENI MWEMBECHAI

ALLY Choki ‘Mzee wa Kijiko’ juzijuzi alikuwa ndani ya ukumbi wa Flamingo, Magomeni Mwembechai akimwaga burudani ya aina yake kwa mashabiki wake wa Kinondoni, hususan wakazi wa eneo hilo.
Muziki ulikuwa wa kutakata sana, ambapo wanamuziki wote wa bendi hiyo walionekana kujituma kikamilifu jukwaani na kuifanya shoo iwe tamu masikioni na machoni mwa waliohudhuria.
Lakini hata hivyo, dosari mbili tatu hazikukosekana, baadhi yake ikiwa ni kama vile Choki mwenyewe kulikimbia jukwaa na kuwaachia ‘madogo’ kwa muda mrefu.
Kadhalika, kana kwamba aliyekuwa akimuiga Choki, nguli Banza Stone naye alitumia muda mwingi kitini kuliko jukwaani na hiyo kuwafanya mashabiki waboleke kwa kiasi fulani.
Hata zilipopigwa baadhi ya nyimbo ambazo nao wameimba kwa kiasi kikubwa, mastaa hao hawakuonekana kabisa jukwaani na hivyo mapengo yao kuzibwa na waimbaji Bob Kisa na Athanas Montanabe.
Ukiondoa hiyo mambo yalikuwa mazuri siku ya jana kwa wapenzi na mashabiki wa waliopata fursa ya kuhudhuria shoo hiyo ambayo kiingilio chake kilikuwa ni kinywaji.
MAMBO YA MASHAUZI CLASSICHASHIM Said ‘Igwe’ mwimbaji pekee wa kiume anayeonekana kumkimbiza kwa kasi Mzee Yussuf ‘Mfalme’ kwenye mipasho,  aling’ara zaidi kwenye shoo ya kundi lake la Mashauzi Classic Modern Taarab.
Shoo hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kuhudhuriwa na zaidi ya mashabiki 250, walioonekana kufurahia vilivyo burudani ya vijana wa Mashauzi wanaotumia mtindo wa ‘Wakali wa Kujiachia’.
Aliimba nyimbo tatu kwa awamu tofauti, ambazo ni zile mbili alizorekodi yeye akiwa na kundi hilo lililo chini ya Mkurugenzi Isha Ramadhani; ‘Bonge la Bwana’ na ‘Niacheni Nimpende’ pamoja na nyingine ya kukopi iitwayo ‘Mazoea Yana Taabu’.
Mbali ya Hashim, wasanii wengine waliofunika kwenye shoo hiyo ya jana ni pamoja na waimbaji Isha mwenyewe, Zubeda Malick, Asia Mzinga, Abdulmaliki Shaaban na Sania Msomali.
Kuonekana kwa mpapasa kinanda Mgeni Kisoda kwenye shoo  ya Mashauzi Classic kumeibua hali ya ‘sintofahamu’ kwa mashabiki waliokuwa na kiu ya kufahamu kama msanii huyo amejiunga rasmi na kundi hilo.
Shoo ya Mashauzi ilipoanza tu, Kisoda alionekana mara kwa mara akipanda jukwaani na kubonyeza vitufe vya kinanda kimojawapo kati ya vile viwili na kushangiliwa na baadhi ya watu wanaomhusudu.
Katika nyimbo nyingine zilizokuwa zikirindimishwa katika ukumbi wa Mango Garden, Kisoda alikuwa akipapasa kinanda kwa staili ya hisia, yaani bila kufuatisha kilivyorekodiwa awali.
Hata hivyo, mashabiki walionekana kufurahia ubunifu huo wa Kisoda ambaye tayari alishapitia bendi kadhaa kubwa, zikiwamo Jahazi Modern Taarab na African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Baada ya shoo kumalizika, mwandishi wa habari hizi alizungumza na Meneja wa Mashauzi Classic, Ismail Sumalaga ambaye hata hivyo hakuwa tayari kuzungumzia suala la Kisoda akidai wakati wake bado.

WASANII NA HAKI ZAO KATIKA KATIBA MPYA, SAFARI YA MAFANIKIO


Kati ya Jumatatu tarehe 25, 26 na 27 Agosti 2014, kundi la wasanii 27 lilifika katika Bunge la katiba kufuatilia mapendekezo yao katika Katiba ambayo waliyoyatoa kuanzia katika hatua za mwanzo za mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi. Kwa kutumia haki anayostahili kila mwananchi wasanii hawa waliweza kukutana na kuzungumza na Mwenyekiti na makamu Mwenyekiti wa Bunge la katiba na baada ya hapo kutembelea na kujieleza katika kamati mbalimbali za Bunge hili. Wasanii wana mambo mawili ambayo wanahitaji yaweko katika Katiba

i.                Wasanii kutambuliwa kama kundi maalumu kama yalivyotambuliwa makundi ya wakulima wafugaji, wavuvi. Sababu za kutaka kutambuliwa huku, ni kuwa kundi hili ni kubwa kuliko hata makundi mengine yaliyotajwa hapo juu. Takwimu za Baraza la Sanaa la Taifa za mwaka 2006 zinaonyesha kuwa wasanii nchini walikuwa kiasi cha milioni 6. Leo ni mika minane imepita na si siri kuwa kundi hili limekuwa na hivyo kukaribia robo ya Watanzania. Kwa bahati mbaya jamii huchukulia neno wasanii kuwa ni wale wa muziki na filamu tu, lakini sanaa ni pan asana na hivyo kuwa na watu wengi sana hata wengine hawajui kama wamo katika kundi hili. Wachoraji, wachongaji, wasusi, wafinyanzi, mafundi sonara, mafundi wa nakshi za aina mbalimbali, wabunifu wa mitindo, waandishi, wapiga piga picha, watangazaji, djs, wahariri, na kazi nyingi ambazo unaweza kujaza ukurasa huu kuziandika, hao wote wanahitaji kutengenzewa taratibu zikiwemo za elimu rasmi ya vipaji vyao, taratibu za ukuzaji na uendelezaji wa kazi hizo na hatimae kuboresha mchango wao wa mapato yao na mapato ya Taifa kwa ujumla.i.              Milikibunifu (Intellectual Property) itajwe rasmi kama moja ya aina za mali zinazohitaji kulindwa katika katika Katiba.  Katika katiba kuna Ibara (Ibara ya 37) inayoongelea ulinzi wa mali. Lakini mali zinazoongelewa hapa ni zile zinazohamishika na zisizo hamishika. Lakini kuna mali muhimu ile isiyoshikika haikutajwa ulinzi wake. Pamoja na kuwa wasanii kwa kawaida hulindwa na hakimiliki, lakini haingekuwa busara kushikilia kipengele hicho tu kutajwa kwenye Katiba, kwani ni sehemu tu ya Milikibunifu ambapo kuna Haki nyingine kama vile ;
·      Patent – (Hataza) hii ni njia ya kulinda na kusajili uvumbuzi mbalimbali wa kiteknolojia. Mfano vifaa vya kuvunia mazao kwa haraka zaidi, au kulima kwa haraka zaidi, vifaa vya uvuvi wa haraka, vifaa vya mawasiliano na vifaa vyovyote ambavyo vitaongeza thamani ya maisha yetu. Katika nchi kama Korea ya Kusini ulinzi wa Milikibunifu uliwekwa katika Katiba kuanzia baada ya vita ya pili ya dunia kwa kufuatia mfumo wa  Katiba ya Marekani na ulinzi huo umeifanya wananchi wake ambao ni wabunifu kuweza kuja naubunifu ambao unatikisa dunia vifaa kama Samsung, Daewoo, KIA, LG ni matokeo ya ulinzi wa kikatiba wa wa Milikibunifu
·      Trademarks – (Alama za Biashara ) Alama za biashara huweza kufikia hatua ambapo zikawa na thamani kubwa kwani huweza kuaminika. Ili kulinda zisitumiwe hovyo au hata kuibiwa na wenye uwezo zaidi hulindwa na sheria za kulinda alama hizi. Kwa mfano Cocacola, Vodacom, Dell, na hapa kwetu Azam, ni majina ya bidhaa ambazo zina aminika, na hivyo kuwa na dhamani kubwa japo hazishikiki, nazo ni sehemu ya mali  ambazo hazishikiki lakini zina thamani kubwa
·      Industrial designs – Hizi ni haki wanazopewa wale wenye ubunifu wa kuweza kufanya usanii wenye kuboresha muonekano wa kitu ambacho tayari kimeshagunduliwa. Kwa mfano kila mtu ana simu ya mkononi lakini muonekano wa simu mbalimbali shape nap engine hali ya kuwa ni ya ku slide au kufungua au kupokea moja kwa moja ni matokeo ya design, pia vitu kama design za nguo, viatu , kiti ulichokalia makochi magari, vyote hivyo ndivyo matokeo ya industrial designs. Kazi za ubunifu huo ni muhimu kulindwa kwani huwa na thamani kubwa sana, kwa mbunifu na kwa mchango wake kwa nchi.
·       Geographical Indication – Huu ni utambulisho wa wapi chanzo cha mali husika. Kwa mfano mvinyo kutoka Dodoma, Dodoma Wine ni mzuri na hivyo huitwa Dodoma Wine bila kulinda hili, watu watachukua mvinyo huu na kuupa hata jina jingine ukaitwa South African wine na hivyo kuiba haki wanazostaili kupata wakulima wa Dodoma, kutambuliwa kwa jina hili kutasababisha kutakiwa zaidi kwa wine hii duniani na hivyo kuweza kufanya hata Dodoma kuwa Wine City jambo ambalo linawezekana lakini nchi haijatambua umuhimu huu. Pia kuna mchele wa Kyela, Dagaa wa Kigoma na vitu kama hivi ambavyo havipatikani popote duniani kasoro sehemu iliyotajwa.  Nchi kama Uswiss imejenga jina miaka mingi ya utengenezaji wa saa bora hivyo saa ikiandikwa Swiss made huwa inajulikana ni bora na huwa gharama zaidi, Sigara kutoka Cuba, Cuban Cigars ni bei kubwa kwani hazipatikani popote kasoro Cuba, au mvinyo maarufu kama Champagne, ambao hutoka jimbo la Champagne Ufaransa, umejijengea sifa kubwa duniani na kuwa na bei kubwa sana kiasi cha kwamba si rahisi kwa mtu wa kipato cha kawaida kununua. Harusi zetu hutumia Sparkling Wine na kuiita Shampeni.
·      Hakimiliki na Hakishiriki – Hizi ni haki zinazolinda kazi za kisayansi na kisanii. Computer Programs, Data, Utunzi wa vitabu, miswaada, hotuba, uchoraji, muziki, kazi za usonara, picha za mnato na filamu, uchongaji na kadhalika. Kazi hizi zimekuwa ni chanzo cha utajiri mkubwa kwa watu binafsi na Mataifa. Katika nchi ya Marekani kazi za Hakimiliki na Hakishiriki ni za pili katika uchangiaji wa pato la Taifa. Ripoti ya WIPO ya 2010 ilionyesha kuwa katika nchi ya Tanzania kazi za hakimiliki na Hakishiriki zilichangia asilimia 4.3 ya pato la taifa, karibu mara mbili ya mchango wa Madini!. Katika mwaka 2009 kazi za hakimiliki zilitengenza aslimia 5.63 ya ajira nchini, ikiwa juu ya mchango wa Afya (4.23), Biashara na mambo ya Fedha Real estate, &Business Service(2.37), Ujenzi (1.38),Usafirishaji na Mawasiliano (0.92), Umeme, Gas na maji (0.91), Madini (0.89) .
Ukiangalia utaona wazi kuwa Milikibunifu ni haki zinazolinda wavumbuzi, watafiti, wanasayansi, wagunduzi wa madawa, ya kisasa na kiasili, wavumbuzi wa mbegu za aina mbalimbali, ulinzi wa alama za biashara hivyo wasanii wameweza hata kuwasaidia wenye viwanda wakulima na wafanya biashara wakubwa katika safari yao hii iliyoanza mwaka jana.
Baadhi ya hasara ambazo Taifa hili limepata kutokana na kutokuwa na taratibu zifaazo katika kulinda Milikibunifu;
a.     Michoro ya Tingatinga milikibunifu yake iko chini ya kampuni ya Walt Disney ya Marekani
b.     Mgunduzi wa Tanzanite ni maskini ambaye amekuwa kwa muda mrefu akijitahidi kupata chochote kutokana na ugunduzi huo ameishia kupata vyeti vya kumtambua  wakati India na South Africa vikitambulika zaidi kuwa chanzo cha madini hayo yapatikanayo Tanzania tu
c.      Ulaghai mkubwa wanaofanyiwa wasanii wa Tanzania kwa kazi zao kutumika masaa 24 na vyombo vya habari wakati wao hawalipwi chochote kwa kisingizio cha promosheni
d.     Wagunduzi wengi kazi zao zikiishia kuonekana kwenye maonyesho tu na hakuna taratibu za kuendeleza kwa kazi hizo wala wabunifu hao
e.     Nchi kukimbiwa na wabunifu wa teknolojia , ambao huona ni heri waende nchi nyingine ambako watathaminiwa, au wabunifu kuacha kufanya ubunifu wowote  kwani hauna faida.


Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...