Skip to main content

Posts

Showing posts from March 7, 2013

MAAJABU YA KABURI LA KANUMBA NA GOBBY

Nilipatwa na mshangao mkubwa baada ya kukumbuka jambo lililosahaulika na pengine kutofahamika kwa wengi la marehemu Isiaka Gobby linalofanana sana na tukio la Steven Kanumba Hatua chache baada ukiingia katika lango la makaburi ya Kinondoni, kushoto kwako utalikuta kaburi la msanii Steven Kanumba. Kanumba akiwa na umri mdogo wa miaka 28, alifariki ghafla katika mazingira ambayo yamepelekea msanii mwenzieElizabeth Michael kuwa katika kesi ya kutuhumiwa mauaji ya msanii huyu aliyekuwa mahiri katika kazi yake ya usanii wa kuigiza na pia aliyekuwa na sura ya kupendeza yenye mvuto, wengi tunamfahamu kwani bado yuko katika mawazo yetu kutokana na kazi zake kuwa bado zikiendelea kuonekana katika vyombo mbalimbali vya utangazaji. Jirani kabisa ya kaburi la Kanumba, kuna kaburi moja la zamani sana la mwanamuziki Isihaka Gobyy.huyu alikuwa mwanamuziki wa Orchestra Makassy katika miaka ya 1976/77. Gobby nae alikuwa na sifa zilizofanana sana na zile za Kanumba. Kwanza alikuwa mwanamuziki muimbaji m…