Sunday, July 24, 2011

Gold All Stars Band

 
Katika zunguka zunguka  yangu nilikutana na bendi hii ambayo ina wanamuziki watatu wa enzi hizo. Nilikuwa napita mitaa ya tandika nikasikia bendi ikipiga wimbo wa Safari Trippers ambao sijausikia siku nyingi sana. Ni ule wenye maneno, 'Hao hao watu fitini, kazi yao kubwa maneno ya uwongo' , nikaona niweke stop. Nika mkuta pia mpiga rythm wa zamani na maarufu Abdallah Gama. Nilimkuta akipiga bezi, nikamkuta pia mwanamuziki ambaye nilimkumbuka kwa jina moja tu Yahaya ambae aliwahi kuwa Msoma Jazz wana Sensera.


Abdallah Gama


Yahaya

JUDITH KIULA MUIMBAJI MPYA WA GOSPEL

Judith Kiula ni mwenyeji wa Singida aliyezaliwa na kukulia Morogoro,  alizaliwa Kizuka hospital, na akaanza shule Kizuka primary school, ...