Skip to main content

Posts

Showing posts from December 19, 2011

Mheshimiwa Waziri Dr E Nchimbi, Serikali haina nia thabiti kumaliza wizi wa kazi za sanaa

KwaMheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo.
WIZI WA KAZI ZA SANAA. Mheshimiwanategemea usalama na unaendelea vizuri na kazi. Mimi si mgeni kwako, nimeshafika ofisini kwako tukaongea mengi sana kuhusu sanaa na hasa wizi wa kazi za sanaa. Ilikuwa ni mapema baada ya wewe kuteuliwa tu kuwa Waziri wa Wizara yetu. Nilitoka ofisini kwako nikiwa na furaha na matumaini, lakini naona muda unakwenda maumivu yako palepale.Nimesikia tena si mara moja hata Mheshimiwa Rais ‘akilaani’ wizi wa kazi za sanaa, lakini kila mara napata picha kuwa serikali haijaamua kumaliza tatizo hili. Mambo mengi yananihakikishia ukweli wa picha yangu hii. Kwa kweli wengine tuliposikia kuwa safari hii wasanii tuko Wizara moja na Habari tukaelewa tatizo letu la kuibiwa na vyombo vya habari litaisha, miezi imepita na sasa miaka inaanza kuhesabika hakuna dalili zozote za kuonyesha mabadiliko ya unafuu wa wizi huo. Hebu tuanze na TBC, chombo ambacho kiko chini ya Serikali yenyewe. Kuanzia katikati ya miaka…