Saturday, July 16, 2011

Gusagusa

Abdul warid- Keyboards


Mariam Shariff


Alifadhil Juma- Keyboards

Mkongwe katika fani nani asiyemjua?Ni Hadji Mohammed guest star katika kundi hili akitokea East African Melody.
Kundi la Gusagusa ni kundi la Taarab ambalo liko tofauti na Taarab nyingine kwa mambo kadhaa. Kwanza kinanda cha kundi hili kimetyuniwa kati ngazi za muziki za Kiarabu(Arabic Scale), tofauti na vinanda vya bendi nyingine ambavyo vimetyuniwa kufwata do re mi fa so la ti. Hivyo ukiingia tu, unapopigwa muziki wa Gusagusa utaona melody zake ziko katika mahadhi ya nchi za Mashariki ya Kati. Pili chombo pekee kinachotumika ni kinanda tofauti na taarabu nyingi hapa Dar zenye magitaa na drums. Siku hizi taarab nyingi zina ule mtindo wa kupiga 'chemka' au kwa Kikongo sebene, Gusa gusa hawako huko. Ni muziki wenye raha kusikia masikioni na wenye waimbaji mahiri akiwemo mkongwe. Gusagusa hupiga Lango la Jiji na Ijumaa huwa Hotel Traventine Magomeni

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...