Monday, May 9, 2011

Taarab ya leo tofauti sana na ya zamani

    
Pozi si kama za zamani

Kucheza si kama zamani
Show nayo ndani

Mavazi nayo yanabadilika

Coast Modern Taarab

DDC Kariakoo saa 5 usiku nililikuta kundi zima  hili la Coast Modern Taarab lenye masikani yake Temeke likitumbuiza baada ya Msondo Ngoma kuwaachia jukwaa. Ni mara ya kwanza kukuta waimbaji wakike wa Taarab wakiwa wote wamesimama mbele ya Maikrofon, taarab inabadilika haswa.
TOT Taarab bado wako hewani

Kati ya vikundi vilivyokuwa ni tishio katika Taarab kwenye miaka ya 90, kundi la TOT lililo chini ya Chama Cha Mapinduzi, lilikuwa mojawapo, naweza kudiriki kusema liliweza hata kuwa ndilo kundi lililopendwa zaidi na wapenzi wa Taarab wakati huo. Likiwa na mpambano mkali na kundi la Muungano Cultural Troupe, na hatimae kubaki peke yake baada ya kundi la Muungano kumeguka, jambo ambalo huwa linasadikiwa lilichochewa na uongozi wa TOT; TOT bado iko hewani na bado ina washabiki wengi. Juzi nililikuta kundi hili likiwa hewani katika ukumbi wa Copacabana Mwananyamala. Na pia kulikuweko na wanamuziki wengine wengi kutoka vikundi vingine vya Taarab hapa mjini.
Malkia Bi Khadija Omar Kopa

Show siku hizi ni sehemu ya TaarabBinti ya Mwanamtama ambae yuko East African Melody

Mwanamtama aka Mama Lao


Bi Aisha alikuwepo aliimba wimbo wake wa Mama

Thabit

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...