Skip to main content

Posts

Showing posts from December 12, 2011

Dushelele wa Ally Kiba na heshima yake katika bendi

Katika muziki kuna njia ya wanamuziki kupeana heshima kutokana na ubora wa kazi au utalaamu. Mara nyingi ukiingia katika onyesho la muziki utasikia wanamuziki wakitambua kuweko kwa mwanamuziki mwenzao aidha kwa kumtaja au kwa kumkaribisha jukwaani ili 'atoe salamu za kisanii'. Hii inaweza kuwa kwa mwanamuziki kushiriki katika wimbo unoendelea au kupiga au kuimba wimbo wake ambao anaona unamtambulisha uwezo wake. Njia nyingine ni kwa wanamuziki kuurudia wimbo wa wanamuziki wengine. Katika nyimbo za wanamuziki wa kizazi kipya, wimbo wa Ally Kiba wa Dushelele ndio wimbo ambao bendi nyingi zimeanza kuupiga katika maonyesho yake katika kipindi hiki. Katika mizunguko yangu nimekwisha sikia bendi tatu zikiupiga wimbo huu vizuri na  katika bendi moja, mpiga solo hutangazwa kuwa yeye ndiye aliyepiga gitaa studio wakati wa kurekodi nyimbo hiyo. Ni wazi ni heshima kubwa kwa Ally Kiba katika jamii ya wanamuziki.

Wahenga walisema cheka Unenepe

MIAKA 50 YA WIZI WA KAZI ZA MUZIKI NCHINI.(Part 1)

Wakati huu wa kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru kuna mengi mazuri ya kukumbuka lakini pia kuna mengi mabaya na ya kusikitisha. Kati ya mabaya kuna mengine yamepita tugange yajayo, lakini kuna mengine yanaendelea na ni lazima tuyaondoe. Kati ya yale ambayo yanasikitisha na ni lazima liondolewe ni hili la miaka 50 ya wizi wa kazi za wasanii. Nchi yetu kama zilivyo nchi nyingine za Afrika ilipitia katika vipindi kadhaa kikiwemo cha kabla ya ukoloni, ambapo msanii alikuwa na nafasi muhimu katika jamii. Msanii alikuwa ni maktaba ya matukio katika jamii, alikuwa ni darasa la jamii, alikuwa ni kiungo muhimu katika matambiko ya jamii, na hata katika matibabu ya jamii na pia mburudishaji wa jamii, na jamii ilimlea kutokana na kipaji chake, na kupewa nafasi ya juu katika jamii. Katika kipindi hicho matumizi ya kazi za sanaa yalikuwa na mipaka kutokana na kazi za sanaa kuwa na malengo na matumizi maalumu, na kutokuweko na teknolojia ya kufanya kazi hizo ziweze kutumika na watu wengi kwa wakati mmoja. …