Thursday, August 4, 2011

Grumet Mamba Band

 Nilikuwa napita maeneo ya Mwenge nikasikia muziki, kilichonivuta sikio langu ni wimbo uliokuwa unapigwa, ulikuwa wimbo wa JKT Kimulimuli ukipigwa 'live'. Baada ya miaka zaidi ya 30 niliusikia tena wimbo huu ukipigwa live. Nikaingia Karabash Bar, nikaikuta bendi  inayoitwa Grumet Mamba Band. Haraka sana nikamuona mpiga kinanda mkimya lakini ana historia kubwa nyuma yake nae ni Kalonda Kapizo. Baba yake Kalonda alikuwa mwalimu wa muziki enzi hizo wakati wa uhai wa Korean Cultural Center. Wanamuziki wengi mahiri walipitia kwa Marehemu Mzee Kapizo. Dada yake Kalonda, Marehemu Joyce Kapizo alikuwa mwimbaji mzuri aliyepitia bendi kadhaa kabla ya mauti yake. Na Kalonda mwenyewe ni kati ya wapigaji bora wa keyboards ninaemfahamu. Kwenye solo gitaa alikuweko Bahati Mpili nae mpiha gitaa mzuri wa miaka mingi, hili kwa kweli lilinipa faraja kuwa muziki 'Live' bado uko hai na utaendelea kuweko kinyume cha mawazo ya wengi sana.
Kalonda Kapizo

Bahati Mpili


Toffy Mbaga

Shaban Mrisho

Albert Semgerere


ToddyNuhu
Kandaya