Skip to main content

Posts

Showing posts from September 8, 2012

TWANGA PEPETA ZIARANI IRINGA NA MBEYA

Bendi maarufu ya African Stars Band maarufu kama Twanga Pepeta itakuwa na ziara ya maonyesho ya nguvu katika mikoa ya Iringa na Mbeya.Tarehe 14-09-2012 siku ya Ijumaa katika Twanga itakuwa katika ukumbi wa Highland. Kesho yake siku ya Jumamosi tarehe 15-09-2012watakuwa Jijini Mbeya ndani ya City Pub na siku ya Jumapili tarehe 16-09-2012 watafanya Bonanza maalum kwa ajili ya wakazi wa Jiji la Mbeya na maeneo ya jirani. Bendi inataraji kuondoka Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa onyesho la kila siku ya Alhamisi tarehe 13-09-2012 litakalofanyika Club Maisha Oysterbay. Twanga Pepeta itakapokuwa katika ziara, itamtambulisha mwimbaji wao mpya Kalala Jr aliyerejea hivi karibuni kutoka katika Bendiya Mapacha Watatu.Sambamba na utambulisho huo pia itatambulisha nyimbo zao mpya za “Ngumu Kumeza” ilyotungwa naMirinda Nyeusi, huyu ni mwanamuziki aliyehamia karibuni kutoka Mashujaa Band, “Nyumbani ni Nyumbani” uliyotungwa na Kalala Jr, “Walimwengu” iliyotungwa na Jumanne Saidna ” Mapambano ya…