Bendi maarufu ya African Stars Band maarufu kama Twanga
Pepeta itakuwa na ziara ya maonyesho ya nguvu katika mikoa ya Iringa na Mbeya. Tarehe 14-09-2012 siku ya Ijumaa katika Twanga itakuwa
katika ukumbi wa Highland.
Kesho yake siku ya Jumamosi tarehe 15-09-2012 watakuwa Jijini Mbeya ndani ya City Pub
na siku ya Jumapili tarehe 16-09-2012 watafanya Bonanza maalum kwa ajili ya
wakazi wa Jiji la Mbeya na maeneo ya jirani.
Bendi inataraji kuondoka Dar es Salaam mara baada ya
kumalizika kwa onyesho la kila siku ya Alhamisi tarehe 13-09-2012 litakalofanyika
Club Maisha Oysterbay.
Twanga Pepeta itakapokuwa katika ziara, itamtambulisha mwimbaji
wao mpya Kalala Jr aliyerejea hivi karibuni kutoka katika Bendi ya Mapacha Watatu. Sambamba na utambulisho huo pia itatambulisha nyimbo zao
mpya za “Ngumu Kumeza” ilyotungwa
na Mirinda Nyeusi, huyu ni
mwanamuziki aliyehamia karibuni kutoka Mashujaa Band, “Nyumbani ni Nyumbani” uliyotungwa na Kalala Jr, “Walimwengu” iliyotungwa na Jumanne
Said na ” Mapambano ya Kipato” uliyotungwa na Kocha wa Dunia, Mwinjuma
Muumini.
Mara baada ya kurejea jijini, Twanga Pepeta itaendelea
kufanya maonyesho yake kama kawaida Jijini Dar es salaam katika kumbi za Club
Billicanas siku ya Jumatano, New Club Maisha siku ya Alhamisi, Free Time Resort
Ukonga Banana, Mango Garden siku ya jumamosi na Jumapili mchana Leaders Club na
usiku Mzalendo Pub.
Comments