Mkataba wa Kumkodisha Msanii, Mwanamuziki au Mwimbaji Msindikizaji kwa ajili ya Onesho la moja kwa Moja (LIVE)
KILA SIKU WANAMUZIKI WANAFANYA KAZI ZA KUFANYA MAONYESHO, JE UNAJUA KUWA NI LAZIMA UPATE MKATABA? JE UNAJUA KUWA LAZIMA KUWEKO NA MKATABA TOFAUTI KWA KAZI YAKO KURUHUSIWA KURUSHWA KWENYE LUNINGA AU REDIO? ANGALIA MFANO HUU WA MKATABA KWA KAZI HIZO. MIKATABA HII IMETAYARISHWA NA UNESCO.
Mkataba huu unaeleza masharti ya
kumkodisha msani kiongozi, mwanamuziki au mwimbaji msindikizaji Kwa ajili ya
kushiriki kwao kwenye onesho la moja kwa moja. Makataba unaeleza wajibu wa
mtayarishaji wa onesho na vilevile wajibu wa wanamuziki na waimbaji
wasindikizaji.
MSANII, MWANAMUZIKI au MWIMBAJI
MSINDIKIZAJI (kwenye makataba huu atarejelewa kama MSANII)
MTAYARISHAJI WA ONESHO LA MOJA KWA
MOJA.
KIFUNGU
CHA 1 – Madhumuni
Bw / Bi. _________________________
anakodiwa kama ____________________________ kwenye onesho lifuatalo la moja kwa
moja _______________________________________ mkataba lazima ujazwe kikamilifu,
pale inapobidi kwa kuzingatia masharti ya sheria za kazi za nchi mkataba
unamosainiwa.
KIFUNGU
CHA 2 – Tarehe na Mahali
Tarehe na mahali pa kufanyia mazoezi
___________________________________________
Wakati
____________________________________________________________________
Tarehe na mahali pa maonesho ya umma
_________________________________________
Wakati
___________________________________________________________________
KIFUNGU
CHA 3 – Kuwahi
Masanii anawajibika kwa mahali pa
kufanyia mazoezi au mahali pa onesho kwa wakati unaotakiwa na ikiwezekana afike
walau dakika kumi na tano kabla ya muda.
KIFUNGU
CHA 4 – Malipo
Malipo kwa kila kipindi cha mazoezi
________________________________________
Malipo kwa kila onesho la wazi
_____________________________________________
KIFUNGU
CHA 5 – Gharama za Usafiri, Malazi na Posho ya kujikimu.
Iwapo MASANII atatakiwa kusafiri na
kuishi kwenye hoteli kwa ajili ya kutekeleza mkataba huu, MTAYARISHAJI
atawajibika.
Ø Kulipa au kurejesha malipo ya usafiri.
Ø Kushika na kulipa moja kwa moja chumba
kimoja cha hoteli, ambamo huduma itajumuisha kifungua kinywa.
Endapo msanii atatakiwa kupata mlo nje
ya nyumbani kwake kwa ajili ya kutekeleza makataba huu, mtayarishaji
atawajibika kumlipa msanii kiasi kisichobadilika cha
___________________________ kwa siku ya safari na / au kwa siku ya kazi.
KIFUNGU
CHA 6 – Rekodi na Matangazo ya kwenye Redio au Televisheni.
Rekodi yoyote na matangazo ya redio au
televisheni lazima yawekewe mkataba maalumu kati ya MSANII na MTAYARISHAJI,
isipokuwa kama utangazaji unafanyika maalumu kwa madhumuni ya promosheni.
Utangazaji unachukuliwa kufanya maalumu
kwa madhumuni ya promosheni, na kwa hiyo MSANII anakubali utangazaji huo, iwapo
muda wa kutangazwa kwa umma hauzidi dakika tatu.
MTAYARISHAJI anawajibika kupata kutoka
kwa mtangazaji uthibitisho kuwa rekodi yoyote ya tangazo linalozidi dakika tatu
haitahifadhiwa isipokuwa kama kuna mkataba maalumu ambao umetiwa saini kwa
kusudi hilo.
KIFUNGU
CHA 7- Mambo Mbalimbali.
Mkataba huu utaongozwa na sheria ya
nchi unamofanyika utayarishaji.
Umesainiwa ……………………….. tarehe …………
katika nakala …………….halisi.
MSANII
_____________________________________
MTAYARISHAJI
________________________________
Comments