Dar Modern Taarab-Pembe la Ng'ombe

Kila Jumanne Dar Modern Taarab huwa pale Copa Cabana Mwananyala wakifanya maonyesho yao, na kila Jumatano kundi hili huwa Lango La Jiji magomeni. Lakini ukingia maonyesho haya mawili utadhani ni vikundi viwili tofauti. Kundi hili limejipanga vizuri sana kiasi kuwa siku ya Jumanne wao hufanya show ya nyimbo zao tu lakini siku ya Jumatano ni siku ambayo umahiri wa kundi hili lenye wanamuziki wakongwe waliowahi kutikisa nchi kutokana na kuwa katika makundi maarufu ya taarab hapa nchini, hupiga nyimbo za zamani tu za Taarab. Siku hii utazisikia nyimbo za zamani kutoka Zanzibar, Tanga, Mombasa, miji iliyona historia ndefu sana ya muziki wa Taarab..... ukweli ukiingia katika onyesho lao saa 5 usiku unaweza kudhani ukumbi hauta kuwa na watu, lakini wapenzi wa kundi hili huwa wamejaza ukumbi ifikapo saa 8 usiku, katika onyesho ambalo huisha alfajiri.


Comments