Marahaba Cultural Festival yafanyika kwa kishindo kikubwa

Lile tamasha la muziki wa kiasili limefanyika katika viwanja vya Biafra na kumalizika kwa kishindo. Vikundi zaidi ya 12 vilipanda jukwaani na kuleta burudani kwa wananchi wakubwa kwa wadogo katika hali ya utulivu mkubwa ambao si kawaida kwa matamasha ya hapa mjini. Hakukuweko na uporaji wala kelele za vilio baada ya muziki, ambapo watu walikuwa watulivu sana na kuonyesha kuwa muziki tofauti una wapenzi tofauti. Tamasha hili lilidhaminiwa na kampuni mbalimbali kama Acqua,Zoom Tanzania, Dream Vision, Insight Security, Chekanakitime Blogspot, Kilimanjaro Bnad Afrikwetu Productions, Cocacola, Javelin Graphics,NB Screen Printing limeanz taratibu baada ya generator kukorofisha kwa muda japo lilifanya kazi njema kwa sa 18 kabla ya tamasha,, hatimae kazi ilianza iliyoweza kuwapa Watanzania waliokuja burudani tamu na tofauti

-->
-->

Comments