Saturday, July 30, 2011

Baikoko

Kundi hili la vijana walioweza kuikubalisha jamii kulipia kwa kuangalia ngoma za asili ni kikundi maarufu katika sehemu nyingi za Dar es Salaam na Tanga. Kundi zima wanatumia vifaa vya kiasili tu. Wakisindikizwa na wanenguaji wawili tu ni kikundi cha kuiona ndo utajua utamu wake hapa walikuwa Dar West Tabata

Mashauzi Classic Modern Taarab

Haya tena nimemkuta Bi Mashauzi Tabata, akiwa katika onyesho lililotayarishwa na promoter wa kike Sauda Mwilima, si mchezo, yeye ndiye muimbaji mkuu kwenye group, na anaimba na kucheza full time. Wasanii wengi hasa wakiwa maarufu hukwepa hilo na kuwaachia 'vijana' halafu mzee anakuja imba nyimbo mbili tatu halafu jiiiii. Big Up Isha endelea hivyo hivyo.JUDITH KIULA MUIMBAJI MPYA WA GOSPEL

Judith Kiula ni mwenyeji wa Singida aliyezaliwa na kukulia Morogoro,  alizaliwa Kizuka hospital, na akaanza shule Kizuka primary school, ...