Skip to main content

Posts

Showing posts from January 3, 2013

UMUHIMU WA UTUNZAJI WA VYOMBO VYA MUZIKI

Jana niliingia katika duka moja la vyombo vya muziki na nikawa na maongezi marefu na mwenye duka, kati ya mambo ambayo tulizungumzia ni tatizo la watu kuamua kufanya shughuli za muziki na kuanza kununua vyombo bila kutaka ushauri wa wataalamu wa mambo ya vyombo vya muziki. Nimeona leo nizungumzie hilo. Kwanza kabisa kumekuwa na tatizo kubwa la kuweko kwa vyombo ‘feki’ katika maduka kadhaa ya vyombo vya muziki. Hivyo si kila chombo kikiwa na nembo ya Yamaha ni kweli chombo kutoka kampuni hiyo, kwa kweli asilimia kubwa sana ya vyombo vya muziki ni feki. Ili kugunduahilo ni muhimu kutumia wataalamu wa vyombo vya muziki. Mfano wa karibu ni mdau mmoja anaeendesha bendi, kujikuta amekwisha nunua vyombo mara 3 katika miaka mitatu kutokana na vyombo anavyounua kutokukidhi viwango vinavyotakiwa. Kwa taarifa zilizopo ni kuwa mara ya kwanza aliuziwa na tapeli aliyejidai katoka Uingereza na vyombo original toka huko, kwa kuwa hakutumia wataalamu alijikuta vyombo alivyovinunua havina sauti yenye u…