Saturday, November 24, 2012

ONYESHO LA KHANGA ZA KALE 2012 LAFANA

Asya Khamsin-Mtayarishaji
Kama ilivyo kawaida katika maonyesho ambayo huandaliwa na Fabak Fashions onyesho hilo lilikuwa na msisimko mkubwa na lilikonga nyoyo za waliohudhuria kutokana na wingi wa ubunifu katika mavazi hayo.ASIA KHAMSIN kwa mara nyingine tena amefanikisha .

MSANII WA FILAMU JOHN MAGANGA AFARIKI DUNIA

RIP JOHN MAGANGA
Kwa mara nyingine tena wiki hii tasnia ya filamu imepoteza msanii mwingine baada tu ya kumaliza mazishi ya Mlopelo. Msanii John Maganga amefariki katika hospitali ya Muhimbili.  Taratibu za mazishi bado zinafanyika.
Ni hivi karibuni tu msanii huyu alisema kuwa amefungua Kampuni yake ijulikanayo kwa jina la Jom Entertainment Co. Ltd, pia akaeleza kuwa alianza kuona kipaji chake tangia mwaka 2001 alipokuwa akifundishwa na msanii nguli wa filamu nchini Ndumbago Misayo 'Thea' ambaye alikuwa mwalimu wake wa maigizo wakati wapo kanisani pale Mwananyamala, baada ya hapo filamu ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Miracle of Love  ambayo ilifanya vizuri sana katika kumtambulisha kisanaa nchini. Mwaka 2008 alishauriwa na ndugu yake Deogratias Shija kufungua kampuni yake kwa ajili ya kuendeleza fani ya filamu, kazi ambazo ziko tayari ni Beautfuls aliyowashilikisha wasanii kama Aunt Ezekier, Haji Salumu 'MBoto' na wengine wengi
Mungu aiweke pema roho ya msanii huyu ambaye ameondoka wakati anaanza kuchipua.

KILICHOJIRI HIP HOP SUMMIT

Mchana kutwa siku ya Ijumaa 23 Nov, wana hip hop na wapenzi wa wadau wa hiphop, walisikiliza maada mbalimbaali na kutoa michango ya mawazo kuhusu maada hizo kati ya waliotoa mada ni Profesa Mitchel Strumpf wa Chuo Kikuu cha dar es Salaam aliyetoa maada Hip Hop Identity and its Struggles Globally, ambapo aliweza kurudi nyuma kwenye hsitoria kujaribu kuonyesha Hiphop ilitoka Afrika na imerudi tena, na alikuwa hata nyimbo kutoka Bukoba zilizorekodiwa kwenye miaka ya 50 ambayo ukisikiliza inashangaza kwani inafanana sana na Hiphop ya leo. Pia alitoa maelezo mengi kuhusu kasheshe ambazo Hip hop inapitia katika sehemu mbalimbali duniani kutokana na tafsiri ya muziki huu. Maada nyingine ilitolewa na John Kitime mwanamuziki wa Kilimanjaro Band Problems and Challenges in the Tanzania Music Sector, maada ambayo iliongelea historia ya muziki wa mapokeo katika Tanzania na matatizo ambayo muziki umepitia na unapitia mapaka wakati huu. Baadhi ya mambo ambayo aliyataja ni Rushwa katika tasnia hii, matatizo ya utekelezaji wa sheria ya Hakimiliki, mahusiano ya historia ya Kisiasa ya nchi hii na muziki na wanamuziki wake, nafasi ya serikali katika maendeleo ya muziki.


Maada nyingine ilitolewa na Charlotte Hill O'Neal aka Mama C aliyetoa maada Tuangalie tulikotoka ili kuweza kusonga mbele. Ambapo katika maada hiyo alitoa mifano ya jitihada za wanaHiphop wa kwanza wa Marekani, katika mazingira yaliyokuwa magumu ya kukosa nafasi ya kazi zao kusikika redioni , na wakati hakukuwa na uwanja huu mpana wa internet. Katika maada yake hii aliongelea kuhusu kituo cha SUA (Saving Underground Artists) kilichopo Arusha na jitihada zake za kuendeleza Hiphop. Mada nyingine iliyotolewa ni  JE WANA HIP HOP WAFANYE NINI ILI KUWEZA KUTOKA ambayo ilikuwa na melezo mengi ya kuonyesha  na kushauri njia mbadala za kuwawezesha wanaHIP HOP kutoka katika mazingira yaliyopo.

HITMA YA MOHAMED IDD aka "CONTROL" WA SIKINDE

HITMA YA MSIBA WA MPIGA GITAA MAHIRI WA MLIMANI PARK ORCHESTRA, MOHAMED IDD aka "CONTROL", ITAKUWA KESHO JUMAPILI NOVEMBA 25, KATIKA UKUMBI WA DDC MWENGE. MKABALA NA LANGO LA KUINGIA MLIMANI CITY

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...