KILICHOJIRI HIP HOP SUMMIT

Mchana kutwa siku ya Ijumaa 23 Nov, wana hip hop na wapenzi wa wadau wa hiphop, walisikiliza maada mbalimbaali na kutoa michango ya mawazo kuhusu maada hizo kati ya waliotoa mada ni Profesa Mitchel Strumpf wa Chuo Kikuu cha dar es Salaam aliyetoa maada Hip Hop Identity and its Struggles Globally, ambapo aliweza kurudi nyuma kwenye hsitoria kujaribu kuonyesha Hiphop ilitoka Afrika na imerudi tena, na alikuwa hata nyimbo kutoka Bukoba zilizorekodiwa kwenye miaka ya 50 ambayo ukisikiliza inashangaza kwani inafanana sana na Hiphop ya leo. Pia alitoa maelezo mengi kuhusu kasheshe ambazo Hip hop inapitia katika sehemu mbalimbali duniani kutokana na tafsiri ya muziki huu. Maada nyingine ilitolewa na John Kitime mwanamuziki wa Kilimanjaro Band Problems and Challenges in the Tanzania Music Sector, maada ambayo iliongelea historia ya muziki wa mapokeo katika Tanzania na matatizo ambayo muziki umepitia na unapitia mapaka wakati huu. Baadhi ya mambo ambayo aliyataja ni Rushwa katika tasnia hii, matatizo ya utekelezaji wa sheria ya Hakimiliki, mahusiano ya historia ya Kisiasa ya nchi hii na muziki na wanamuziki wake, nafasi ya serikali katika maendeleo ya muziki.


Maada nyingine ilitolewa na Charlotte Hill O'Neal aka Mama C aliyetoa maada Tuangalie tulikotoka ili kuweza kusonga mbele. Ambapo katika maada hiyo alitoa mifano ya jitihada za wanaHiphop wa kwanza wa Marekani, katika mazingira yaliyokuwa magumu ya kukosa nafasi ya kazi zao kusikika redioni , na wakati hakukuwa na uwanja huu mpana wa internet. Katika maada yake hii aliongelea kuhusu kituo cha SUA (Saving Underground Artists) kilichopo Arusha na jitihada zake za kuendeleza Hiphop. Mada nyingine iliyotolewa ni  JE WANA HIP HOP WAFANYE NINI ILI KUWEZA KUTOKA ambayo ilikuwa na melezo mengi ya kuonyesha  na kushauri njia mbadala za kuwawezesha wanaHIP HOP kutoka katika mazingira yaliyopo.

Comments