Wednesday, June 22, 2011

Schengen Band wakiwa Mango Garden Kinondoni

 

Nilipoingia tu katika ukumbi  wa Mango Jumapili nilikaribisha na Bingwa wa salamu wa zamani ambae kwa muda mrefu amekuwa rapa katika bendi mbalimbali na sasa ameanza hata kuimba katika kundi hili la Schenge nae si mwingine ila ni Loboko Lobi Papaa

Mwendapole fundi mitambo karithi kipaji cha marehemu baba yake


Rais wa Bendi Liva Hassan
The East African Melody Lango la Jiji

Si vikundi vingi vinavyoweza kufanya maonyesho siku ya Jumatatu, hasa kwa kuwa ni wazi vitakosa watu, lakini East African Melody hufanya onyesho Jumatatu katika ukumbi wa Lango la Jiji Magomeni na kwa kweli ni sawa kabisa kusema huwa hakuna hata mahala pa kutema mate. Muziki safi . mirungi kwa wingi mabinti wamevaa kila aina ya nguo basi ni burudani sana. Bi Mkubwa Mwanahawa alikuweko katika onyesho la kundi hili ambalo liliwahi kutikisa jiji na kibao chake KINYAGO CHA MPAPURE
Muimbaji mpya wa TOT Omary Ally

 Omary Ally ni kijana mdogo ambae ameanza kuimba karibuni katika kikundi cha Taarab cha Tanzania One Theatre. Pamoja na kuwa ni bado mchanga katika fani, Omary anaonekana wazi atakuwa tishio kwa wanamuziki wengine vijana katika fani hii.

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...