Saturday, October 20, 2012

26 Oktoba Marahaba Cultural Festival Viwanja vya Biafra Kinondoni

Tanzanian Cultural Organization inawakaribisha wooote katika viwanja vya Biafra,  Kinondoni on 26th Oct 2012, kuanzia saa 6 mchana na kuendelea kusherehekea Tamasha la Marahaba Cultural Festival. BUREEEEEEEEEEEEE
Unakaribishwa uone kazi za sanaa za mikono za ubunifu mbali mbali wa kiasili wakati muziki ukiendelea jukwaani utakaopigwa na wasanii kama Afrikwetu Band, Segere Original, Jhiko man, Yvonne Mwale kutoka Zambia, Gladys Muthue Keetu wa Kenya, Jipe Moyo toka Dodoma na wasanii wengine mbalimbali, si kitu cha kukosa.

Aunt Ezekiel 'aolewa'

 
Msanii wa filamu nchini, maarufu kwa jina la Aunt Ezekiel amefunga ndoa Alhamisi Oktoba 18 2012 maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, katika iliyohudhuriwa na ndugu, jamaa na rafiki zake.
Aunt alifunga ndoa ya Kiislam na  Sunday Demonte anayefanya shughuli zake za kibiashara huko Dubai, japo Sunday mwenyewe hakuwepo bali aliwakilishwa na ndugu. Sherehe kubwa inategemewa kufanyika baadae huko Dubai.

VIJANA WA TANZANIA HUENDA WAPI KUPUMZISHA AKILI BAADA YA SAA ZA KAZI?

AWALI HAPA PALIKUWA NA JENGO LILILOITWA  NYUMBA YA SANAA WASANII WENGI WALIKUWA WAKIFANYA KAZI ZAO HAPA, KWA SASA KILICHOBAKI JINA WASANII...