Skip to main content

Posts

Showing posts from November 12, 2013

MADANSA WATENGENEZA CHAMA CHAO

Madansa wa Tanzania ambao ni maarufu kwa jina la ‘ wacheza show’ hatimae wameweza kuunda chama chao Tanzania Dancers Association, ambacho si tu kina uongozi wa Kitaifa lakini pia tayari kina matawi ya kiwilaya. Jambo ambalo vyama vingi vya sanaa havijaweza kufikia. Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hiki ni Bi Husna Katibu wake akiwa ni dansa maarufu Chino Loketo.
Jumatatu hii chama hiki kilifanya mkutano mkubwa na kumkaribisha Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki kuwa mgeni rasmi wa mkutano wao huu mkubwa uliofanyika pale Garden Breeze Magomeni. Pamoja na John Kitime pia walialikwa wanamuziki maarufu kama Waziri Ally wa Kilimanjaro Band, Nyosi El Saadat Rais wa FM Academia, Ally Chocky Mkurugenzi wa Extra Bongo, na Hussein Tendega maarufu kama Hussein Macheni. Katika kikao hiki, Nyoshi alitoa mchango wake kwa chama wa shilingi laki moja, na Ally Choky aliahidi laki mbili, Hussein Macheni pia aliahidi laki mbili. Hussein Macheni amekuwa kiungo kikubwa kwa madansa hawa kwa kuwa wakati akiend…