Skip to main content

Posts

Showing posts from December 4, 2016

KUMBUKUMBU ZA KUWA MWANAMUZIKI KATIKA AWAMU MBALIMBALI ZA NCHI HII

Karibu kila kituo cha redio siku hizi kina kipindi maalumu cha muziki wa zamani. Nyimbo na hadithi za matukio ya wanamuziki enzi hizo zimekuwa zikiongeza wasikilizaji wa rika zote bila kujali jinsia. Lakini hali ilikuwaje kuwa mwanamuziki enzi hizo? Nina bahati ya kuwa mwanamuziki katika awamu za marais wote waliowahi kuongoza nchi hii, na hakika kumekuwa na tofauti za maisha katika katika kila awamu. Nilianza kujihusisha na muziki katika vikundi mwishoni mwa miaka ya 60 wakati nilipoingia sekondari. Enzi ya Mwalimu. Wakati huo shughuli za sanaa kwa ujumla zilikuwa na nafasi muhimu katika elimu. Wachoraji, wachongaji, wanamuziki walipewa nafasi ya kukuza na kuonyesha vipaji vyao, shule zilitoa nafasi maalumu kwa shughuli hizo. Hivyo nikiwa ‘Form One’, wakati huo neno ‘Kidato’ lilikuwa halijulikani, na wenzangu tulianzisha ‘bendi’ yetu. Shule yetu ikatukabidhi ‘Tape recorder’ tufanyie mazoezi na pia kujirekodi. Mashine hii ilikuwa na uwezo wa kuwa amplifaya hivyo tuliweza kuunganisha m…