Monday, March 11, 2013

DIJITALI YALETA TABU LAKINI VYOMBO VYA UTANGAZAJI ANZENI KULIPA MIRABAHA KWA MATUMIZI YA KAZI ZA SANAA

WAKATI WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI WAKIDAI HAKI YAO SWALI LINAFAA KUULIZWA JE,KWANINI HAWAJAWAHI KUANZA KUWALIPA WASANII KWA KAZI WANAZOZITUMIA KUPATA MABILIONI YA FEDHA ,JAPOKUWA REGULATIONS ZA HAKI HIYO ZIKO TAYARI TOKA 2003? JAMBO AMBALO WAO HUJITETEA NI KUWA HAWANA PESA ZA KULIPA, HILI NI UTATA (KWA KUTUMIA NENO LISILO LA MAKALI),KWA KUWA WENYE MATANGAZO NDIO WANAOSTAHILI KULIPA KWA MATUMIZI YA KAZI ZA SANAA, HIVYO VYOMBO VYA HABARI NI WASAIDIZI WA WASANII KATIKA KUKUSANYA HAKI ZAO, BADO WANANG'ANG'ANIA KUTUMIA KAZI ZA SANAA BURE KWA KILA KISINGIZIO.

ASHA BARAKA AJITAYARISHA KUFUNGUA STUDIO KUBWA

Mwanamama maarufu kwa jina la Iron Lady, Bi Asha Baraka ambaye kwa miaka mingi amekuwa katika biashara ya muziki ameanza kuandaa hatua nyingine ya katika tasnia hii kwa kuwa katika matayarisho makubwa ya studio kubwa mpya itakayokuwa na idara ya video na audio, na hivyo kuweza kurekodi muziki na kutengeneza filamu. Studio hiyo iliyoko maeneo ya Vijana Social Hall Kinondoni, italeta changa moto mpya kwa wadau wote wa muziki nchini. Nilipata bahati ya kuruhusiwa kuingia kwenye studio hiyo ambayo sehemu kubwa bado iko katika matayarisho
Chumba cha 'sound engineer'
Asha Baraka akiwa nje ya studio yake mpya, pamoja nae ni meneja maarufu wa bendi Zonte

Chumba cha editing cha filamu

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...