Skip to main content

Posts

Showing posts from December 18, 2012

WASANII WALETA MTAFARUKU MKUBWA KWENYE MKUTANO NA TRA..

Semina ya TRA ya URASIMISHAJI WA TASNIA YA MUZIKI NA FILAMU, imeisha kwa kusambaratika bila kuagana rasmi kutokana na wasanii kuja juu na kuuliza maswali ambayo majibu yake hayakuwaridhisha wasanii.Hivyo kuzuka mtaafaruku mkubwa katika ukumbi. Semina hiyo ambayo ilitangazwa kuwa ingekuwepo katika ukumbi mkubwa wa Jumba la Makumbusho ya Taifa katikati ya Jiji la Dar es salaam ilikuwa imepangwa ianze saa nne lakini ilichelewa na kuanza saa 5. Wasanii mbalimbali, vijana na wazee wa filamu na muziki wakisindikizwa na viongozi wa vyama na Mashirikisho yao walikuwemo. Kwa upande wa serikali kulikuweko na Maafisa kutoka Ukurugenzi wa Utamaduni, BASATA, COSOTA, Bodi ya Filamu wakiongozwa na TRAambao ndio walikuwa wasemaji wakuu. Semina ilianza kwa maelekezo kuhusu nini kitakachofanyika ili kuanza kuhakikisha stika za TRA zimebandikwa kwenye kila kazi ya sanaa(CD,DVD,Kanda na kadhalika). Kwa maelezo  ya muwezeshaji hili lingeleta faida kwa kulinda haki za wasanii. Iliilezwa kuwa taratibu hizi…