Skip to main content

Posts

Showing posts from July 17, 2011

EXCEL Band kazini

Hawa utawakuta Swiss Pub Tabata kila Jumapili.


Mayama Sound Band

Nimeikuta Band hii ikipiga kwenye bar ya Red October Tabata, ni bendi iliyochanganyika vijana na wakongwe. Mpiga Bass gitaaKassim Mafanya aliwahi kupigia bendi ya Uhamiaji iliyokuwa na staili ya Hamahama. Mpiga rythm uma ni mdogo wake Mzee Makelo ambae alikuwa mpiga solo mahiri enzi za Butiama Jazz Band.

TWANGA PEPETA NA MSONDO KUMCHANGIA NGURUMO MATIBABU.

Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta”  imepanga kufanya onesho maalum kwa ajili ya kumchangia fedha za matibabu mwanamuziki mkongwe wa Bendi ya  Msondo Ngoma Music Muhidin Ngurumo.
Onyesho hilo maalum linataraji kufanyika katika ukumbi wa Mango Garden uliopo Maeneo ya Kinondoni hapa Jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi tarehe 23-07-2011.
Burudani inataraji kutolewa na Twanga Pepeta yenyewe sambamba na Msondo Ngoma wenyewe na sehemu ya mapato ya onyesho hili yataenda kwa ajili ya kumchangia Mzee Ngurumo matibabu yake. Pia Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 Mary Khamis anataraji kuonesha ustadi wake katika kusakata mitindo ya Twanga Pepeta.
Sehemu kubwa ya maandalizi yamekwisha kukamilika ili kufanikisha onyesho hilo na Twanga Pepeta itatumia onyesho hilo kwa ajili ya kutangaza albamu yake mpya inayotarajiwa kutambulishwa hapo baadae mwaka huu. Nyimbo zilizomo kwenye albamu mpya ya Twanga Pepeta ni pamoja na Kauli, Kiapo cha Mapenzi, Umenivika Umasikini, Mtoto wa Mwisho, Dunia Daraja na Penz…