Skip to main content

Posts

Showing posts from February 19, 2014

HARAKATI DODOMA

HARAKATI ZA WASANII KUPATA NAFASI KATIKA KATIBA MPYA—3

Kamati ilipata mapokezi ya heshima kubwa kutoka kwa wabunge wa CHADEMA, ambapo Wabungesita wa CHADEMA walikaa na kuwasikiliza wawakilishi hawa wa wasanii wakieleza mapendekezo yao katika Katiba kuhusiana na wasanii. Wasanii wana ajenda mbili, 1. Kundi la wasanii kutajwa katika Katiba kuwa ni kundi rasmi kutokana na ukubwa wa kundi hili nchini, kama yalivyotajwa makundi ya wakulima, wafugaji, wavuvi na kadhalika, pia mchango wake katika ajira ya vijana na ukubwa wa pato linalotokana na kundi hili, ambalo kutokana na kutokutambuliwa linapotea katika mifuko ya watu na kukosesha wasanii na Taifa pato kubwa.  2. Wasanii walitaka ubunifu ulindwe kwanza kwa ulinzi wa Milikibunifu kutajwa rasmi katika katiba na hivyo kuwezesha sheria bora kutungwa na pia utekelezaji wa ulinzi wa kazi zao uweko kama ilivyo katika mali nyingine za wananchi wengine. Kikao cha saa moja na nusu kilikuwa cha mafanikio na kuwa na faida kwa pande zote mbili. Wasanii hawakulala mapema kwani walimalizia siku na kuha…

HARAKATI ZA WASANII KUPATA NAFASI KATIKA KATIBA MPYA—2

Ili kuwezesha kufika Dodoma na kuwakilisha mapendekezo yaliyokusanywa na Mashirikisho, Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET), waliwezesha idadi ya wasanii 12 kufika na kuishi Dodoma. Wasanii hao wakiwemo viongozi toka Mashirikisho wameza kufika Dodoma na kuanza kazi mara moja ya kukutana na Wabunge mbalimbali, na kufanya nao mikutano na mazungumzo ya papo kwa popa na kwa kweli mapokezi yamekuwa ya hali ya juu yanayoleta tumaini kubwa kwa  wote waliofika huku. Wasanii waliomo katika msafara huu muhimu kwa tasnia na Taifa ni


1.Simon Mwakifwamba – Rais, Shirikisho la Filamu (TAFF)
2.John Kitime – Mwenyekiti, Tanzania Musicians Network (TAMUNET)
3.Bishop Hiluka – Katibu Mkuu, TAFF
4.Yobnesh ‘Batuli’ Yusuph –Msanii/FilmProducer
5.Samwel ‘Braton’ Mbwana –Tanzania Urban Music Association (TUMA)/Music Producer
6.Paul ‘P Funk’ Matthysse – Mwenyekiti, Tanzania Producers Association/ Producer
7.Kulwa ‘Dude’ Kikumba – Msanii/ Producer
8.Abdul Salvador –Katibu Mkuu, Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF…