Saturday, July 23, 2011

Pamoja na kukosa umeme wa Tanesco muda wote onyesho la Sauti za Kale lapendeza

Pamoja na kukosa umeme wa TANESCO kwa muda wote ambao onyesho lilifanyika na hivyo kusababisha robo tu ya vyombo kutumika onyesho kwa ujumla lilifana. Kutokufanya kazi vizuri kwa vyombo kulifanya watu wapate asilimia 80 tu ya kilichotayarishwa . Kwa ujumla onyesho lilifanikiwa na video za onyesho zitakuwa sokoni karibuni


DANNY MWAKITELEKO HATUNAE TENA


MHARIRI wa gazeti la Rai, ambaye pia ni Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari, Danny Mwakiteleko ,hatunae tena Mungu amempenda zaidi. Mwakiteleko amefariki leo alfajiri katika hispitali ya Muhimbili. Mwakiteleko alilazwa katika kitengo cha watu mahtuti Muhimbili baada ya ajali aliyoipata juzi usiku (jumatano) eneo la Tabata (ToT), katika ajali hiyo gari alilokuwa akiendesha Mwakiteleko aliingia chini ya  lori lililokuwa kando ya barabara. MUNGU amlaze pema
 Amen

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...