Skip to main content

Posts

Showing posts from March 10, 2012

Mchawi wa vyama vya muziki ni wanamuziki wenyewe-Part 1

Katika historia ya muziki hapa nchini, kumekuweko na vyama vingi vya muziki. Miaka ya nyuma kulikuweko na vyama kama Dar es Salaam Musicians Association, baadae wakati lilipokuweko Baraza la Muziki la Tanzania(BAMUTA), kulianzishwa vyama kama Tanzania Taarab Association(TTA),  na  Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA). Baadae katika enzi ya Baraza La Sanaa La Taifa, kumekuweko vyama kama Tanzania Folk Music Development Association(TAFOMUDEA), Tanzania Rappers Association (TRA), Tanzania Women Musicians Association(TAWOMA), Union of Tanzania Musicians (UTAMU),Tanzania Disco Music Association (TDMA), Tanzania Musicians Network (TAMUNET), Tanzania Urban Music Association (TUMA) na vingine vingi. Pia siku hizi kuna Shirikisho la Muziki Tanzania ambalo linategemewa kuwa ni muungano wa vyama vyote vya muziki nchini. Pamoja na idadi kubwa ya vyama vya muziki kama ilivyotajwa hapo juuni vyama vichache sana ambavyo vimetajwa vinaweza kuitwa viko hai. Bila kusita nasema kuwa wachawi wa…