Skip to main content

Posts

Showing posts from May 17, 2012

Donna Summer hatunae tena

LaDonna Adrian Gaines aliyejulikana zaidi kwa jina la Donna Summer amefariki leo Key West Florida akiwa na umri wa miaka 63. Donna Summer amefariki kwa tatizo la Kansa.  Donna alizaliwa tarehe 31 December 1948. LaDonna alikuwa mmoja wa watoto saba katika familia yao iliyokuwa inaishi Boston, Marekani, mwaka 1971 Donna akahamia Austria ambapo alikutana na Helmuth Sommer ambaye walicheza wote sinema ya Godspell, na wakaoana 1973 walipata mtoto mmoja lakinindoa ilivunjika 1975. Dona alichukua jina la huyo mumewe aliyekuwa Mjerumani na kulitafsiri jina kwa Kiingereza na akapata jina la Summer ambalo ndilo lilikuwa jina lake la jukwaani. Mwala 1978 wakati anatayarisha kibao cha ‘heaven Knows’ ndipo alipokutana na Bruce Sudano na wakaoana July 16, 1980, japo 1979 walipata mtoto wao kwanza, mtoto wa pili alizaliwa 1981. Pamoja na nyimbo zake kuigwa na wanamuziki wengi kama Madonna, Whitney Houston, Diana Ross, Britney Spears, na ule wa "Love to Love You Baby" ulikuwa sampled na…