Friday, April 22, 2011

Wanamuziki wa Njenje watembelea mazoezi ya Yakwetu Band

Katika kuonyesha ukaribu wa kimuziki, bendi mpya ya Yakwetu iliwakaribisha wanamuziki wa Kilimanjaro Band WanaNjenje kwenye mazoezi yao kabla ya kwenda studio. Baada ya kufanya show Waziri Ally wa Njenje alikuwa na haya ya kusema, "Bendi nzuri, waimbaji excellent, lakini inaonekana lazima wafanye arrangement ya kuweza kuoanisha drums na ngoma zile za kiasili, pia Keyboards na Marimba zipangwe ili sauti zioane. Bass guitar na bass drum bado zinagongana". Wanamuziki walikubaliana na hilo kwa kusema walikuwa hawajilipa muda bado hilo, hivyo kuanza kulifanyia kazi mara moja.


Waziri Ally na Mohamed Mrisho wakisikiliza nyimbo za Yakwetu Band

Mabinti wanaoshindania Kimwana wa Twanga Pepeta wako katika mazoezi makali


Kassim Mohammed "Super K" na  Husna Idd au "Sajent"
Mabinti 20 wameanza mazoezi makali kwa ajili ya mpambano wa Kimwana wa Twanga Pepeta 2011. Mazoezi hayo yako chini ya Kongozi wa shoo ya Twanga Pepeta Kassim Mohammed au "Super K" wakisaidiana na Matron Husna Idd au "Sajent" ambaye ni mshindi wa pili wa shindano la mwaka 2007.
 Utambulisho wa washiriki unataraji kufanyika katika Klabu ya San Siro siku ya ijumaa ya tarehe May 3 2011, kukiwa na  burudani itakayotolewa na 20% pamoja na Twanga Pepeta. Nusu Fainali itafanyika Ijumaa 27 May, 2011 katika Klabu ya San Siro na fainali zitakuwa Ijumaa 3 June, 2011. 


Mabinti mazoezini

Mugongomugongo

Wanamuziki wa Tanzania nje-Jibal Band

Katika mji wa Muscat, vikundi vingi vya muziki kutoka Tanzania vimekuwa vikifika na kufanya masikani. Bendi kama Tanzanite, Kilimanjaro, InAfrika, African Stars, African Beat, na nyingi nyingine zimepita katika mji huu. Kati ya bendi ambazo zimekuwa huko kwa muda mrefu ni Jibal Band, yenye wanamuziki kama Amour Saleh Amour maarufu kama Zungu ambaye amewahi kupigia kinanda bendi za Twanga Pepeta, TOT, DoubleM, Edson Teri aliyeanza kupata umaarufu katika kile kipindi cha Bongo Star Search na kupitia Band kadhaa baada ya hapo, ikiwemo African Beat ya Mafumu Bilali, mpiga gitaa Bonzo Kwembe na  wenzao, wamekuwa katika ukumbi  wa hotel ya Ramee Dream wakipiga muziki karibi kila siku, wakisindikizwa na show safi ya nguvu hapa ni baadhi ya wanamuziki hao
Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...