Wanamuziki wa Njenje watembelea mazoezi ya Yakwetu Band

Katika kuonyesha ukaribu wa kimuziki, bendi mpya ya Yakwetu iliwakaribisha wanamuziki wa Kilimanjaro Band WanaNjenje kwenye mazoezi yao kabla ya kwenda studio. Baada ya kufanya show Waziri Ally wa Njenje alikuwa na haya ya kusema, "Bendi nzuri, waimbaji excellent, lakini inaonekana lazima wafanye arrangement ya kuweza kuoanisha drums na ngoma zile za kiasili, pia Keyboards na Marimba zipangwe ili sauti zioane. Bass guitar na bass drum bado zinagongana". Wanamuziki walikubaliana na hilo kwa kusema walikuwa hawajilipa muda bado hilo, hivyo kuanza kulifanyia kazi mara moja.










Waziri Ally na Mohamed Mrisho wakisikiliza nyimbo za Yakwetu Band

Comments

Anonymous said…
Ni mfano mzuri sanana unao poswa kuigwa, kwa wanamuziki wachanga wanaopenda maendeleo kuwaalika wanamuziki wakongwe kuja kutoma maoni yao kabla ya kutoa kitu halisi. Kwa njia hii na ushirikiano huu bila ya shaka band hii inaweza kuwa miongoni mwabendi bora ninazotitambua mimi ambazo ni Njenje, inafrica na band anayoshiriki Rashid pembe. Vijana hawa wanatakiwa kuzingatia ushauri makini toka kwa bwana waziri ally aka mzee wa nyonga.