Sunday, October 21, 2012

MSANII LORD EYES ATUHUMIWA WIZI NA MSANII MWENZIE OMMY DIMPOZ

Habari ambazo si nzuri kutokea wala kuandika, hatimae zimetokea, msanii Ommy Dimpoz kupitia akaunti yake ya twitter ametweet kwamba amemkamata rapper wa Nako 2 Nako Lord Eyes akiiba vifaa mbalimbali vya gari yake. Pamoja na mengine Ommy aliongeza kuwa Lord amekuwa akifanya mchezo huo kwa watu wengi. Ilikuwa ikijulikana kuwa kwa muda mrefu Lord Eyes alikuwa mpenzi wa RayC ambae inadaiwa anasumbuliwa na matatizo ya madawa ya kulevya. Kuna mengi ya kujifunza kwa wasanii wengine katika habari hizi

MOHAMED IDD CONTROL AFARIKI DUNIA


TANZIA, Mpiga gitaa mahiri MOHAMED IDD aka "CONTROL" amefariki dunia leo alfajiri. Wakati wa uhai wake marehemu amewahi kupigia bendi kadhaa zikiwemo Double O ya King Kiki,  National Panasonic, Mlimani Park, OTTU na alienda kufanya kazi Uarabuni na  Zanzibar Sound ya Asia Darwesh. Baada ya kukaa Uarabuni kwa muda aliamua kurejea bendi yake ya zamani ya Sikinde. Miongoni mwa vibao vilimpatia umaarufu ni pamoja na wimbo Gloria wa OTTU ambao alipiga solo. R.I.P IDD CONTROL