Tuesday, April 19, 2011

Mapacha watatu -Coco BeachMafumu na saxSura nzuuriii
Nimewakuta Mapacha Watatu wakipiga Coco Beach, kwa ukweli nimependa uimbaji, utunzi na upigaji wa vyombo. Nimemkuta na ndugu yangu Mafumu Bilali akipiga sax kwenye baadhi ya nyimbo japo yeye ana bendi yake African Beat, huu nao ni mtizamo mpya hongera kwa wote. Stage show yao ina wasichana wazuri kwa sura na pia wachezaji wa ukweli.

Manywele Kimwana wa Twanga PepetaLulu Semagongo mshindi wa 2006
Halima Harun mshindi wa 2007
KAMPUNI ya Manywele kwa kushirikiana na The African Stars Entertainment wamezindua rasmi shindano la kumsaka Kimwana wa Twanga 2011. Shindano litatambulishwa rasmi Mei 6, 2011, katika ukumbi wa Club Sunciro Sinza Dar es Salaam. Mshindi kwenye shindano hilo safari hii atazawadiwa  duka la vipodozi lenye thamani ya sh. Milioni 5. Form za ushiriki zinapatikana kila wanapopiga Twanga Pepeta, Steers, Duka la Manywele na ofisi za Aset Kinondoni. Hii itakuwa ni mara ya tatu shindano hili linafanyika.2006, 2007 na sasa 2011.

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...