Skip to main content

Posts

Showing posts from August 18, 2014

MBARAKAH OTHMAN WA SIKINDE AONJA JUKWAA LA MSONDO

MPULIZAJI tarumbeta mkongwe, Mbaraka Othman amefichua kuwa, anaichukia kupita kiasi bendi ya Msondo Ngoma Music, licha ya jana kuonekana kupanda kwenye jukwaa lao na kushiriki kupiga baadhi ya vibao vya zamani. 
Mbaraka aliyasema hayo jana, muda mfupi baada ya kutelemka kwenye jukwaa la Msondo alipopanda na kusaidia kupuliza tarumbeta kwenye vibao ‘Piga Ua Talaka Utatoa’, ‘Kaza Moyo’ pamoja na ‘Kilio cha Mtu Mzima’.
Huku akishangiliwa na baadhi ya mashabiki, Mbaraka alipanda kwenye jukwaa la Msondo majira ya saa 7:00 usiku na kujiunga na wapulizaji tarumbeta wa bendi hiyo, Roman Mng’ande, Hamis Mnyupe pamoja na mkali wa Domo la Bata, Shaaban Lendi.
“Nimepanda kujifurahisha tu, lakini sina mpango wowote na bendi ya Msondo,” alisema Mbaraka alipoulizwa kama ana nia ya kujiunga na Msondo.
Alisema, alikuwa anarudi nyumbani kwake jirani na hapo walipokuwa wakitumbuiza Msondo, akitokea DDC Kariakoo wakati huo, baada ya kumaliza shoo na bendi yake ya Mlimani Park Sikinde, ndipo alipokatiza ku…

INSPEKTA HARUN ASEMA ANA NDOTO ZA KUJIUNGA NA BENDI KUBWA YA DANSI

UKUMBI wa Sun Diego, Tandika, jijini Dar es Salaam jana ulilipuka furaha ghafla baada ya staa wa Bongofleva, Haroun Kahena ‘Inspekta Haroun Babu’ kuvamia jukwaa la bendi ya JM Mbeta iliyokuwa ikitumbuiza na kuimba nyimbo kadhaa za dansi za zamani.
Kama sinema vile, Inspekta aliyeingia ndani ya ukumbi huo muda mfupi baada ya ratiba ya Mbeta Band kuanza, alikwenda kutulia kwenye meza iliyokuwa pembeni kidogo, kabla ya Kiongozi wa bendi hiyo mwanamuziki mkongwe Julius Mzeru kumkaribisha jukwaani kusalimia.
Akionyesha kujiamini kupita kiasi, Inspekta alipopanda jukwaani alikamata kipaza sauti akatoa salamu kwa mashabiki pamoja na kuwashukuru Mbeta Band kwa kumpa heshima hiyo, kisha akaomba apigiwe kibao chochote alichoimba Bichuka.
Kama waliopanga vile, mara moja wanamuziki wa Mbeta wakaanzisha ala ya wimbo ‘Siwazuri Binadamu’ wa bendi ya OSS na kujikuta wamewainua watu na kuwavuta kati kucheza, huku wengine wakipigana vikumbo kumtuza Inspekta aliyekuwa akiimba kwa hisia kali.
Baada ya wimb…