Tuesday, June 18, 2013

SAIDA KAROLI ASEMA SINA MPANGO WA KUFA BADO

SAIDA VERY
-->
Baada ya taarifa kuzushwa kuwa Saida Karoli amefariki katika ajali ya meli habari za uhakika ni kuwa Saida Karoli wala hayuko mahala popote jirani na Ziwa  Victoria. Baada ya kuweko Dar es Salaam wiki iliyopita, Saida na kundi lake walikodishwa na kuelekea Makongorosi Chunya mahala aliko mpaka asubuhi hii. Saida Karoli anasema hana mpango wowote wa kufa KARIBUNI. 
MUNGU AMUONGEZEE SIKU NYINGI ZENYE FARAJA KATIKA MAISHA YAKE

HABARI ZIMEENEA KUWA INAHOFIWA SAIDA KAROLI AMEFARIKI DUNIA

Kutokana na maelezo kutoka blog mbalimbali ikiwemo Mjengwa Blog na Sundayshomary.com mwanadada muimbaji aliyekuwa kipenzi cha Watanzania mara baada ya kutoa wimbo wake Chambua kama karanga, Bi Saida Karoli amefariki dunia baada ya chombo alichokuwa akisafiria kutoka kisiwa cha Goziba kuzama baada ya kupigwa na dhoruba kubwa. Bado habari zaidi hazijapatikana hivyo tunasubiri habari za ziada na kuweza kuwapasha wapenzi wa mwanadada huyu.

JUDITH KIULA MUIMBAJI MPYA WA GOSPEL

Judith Kiula ni mwenyeji wa Singida aliyezaliwa na kukulia Morogoro,  alizaliwa Kizuka hospital, na akaanza shule Kizuka primary school, ...