Friday, September 23, 2011

Aslay- na NAKUSEMEA, kipaji cha hali ya juu

Bila wasiwasi ASLAY kutoka katika kampuni  ya Mkubwa na Wanawe TMK, ana sauti yenye ukomavu kuzidi umri wake wa kimaisha ya muziki. Mwimbaji mzuri ni yule ambaye anapoimba we msikilizaji unapata hisia ya ujumbe anaoutuma. Aslay ananikumbusha sifa aliyokuwa akipewa Michael Jackson alipokuwa mdogo, alikuwa akiweza kuimba kwa hisia ambayo kwa kawaida hutokana na kupitia machungu au furaha unayoiimba. Nalisikia hilo katika sauti ya Aslay. Namuombea Mungu kijana huyu aepuke na ulevi wa aina yoyote ile ili aweze kufaidi kipaji hiki ambacho Mola amemjalia, kwani kwa sauti hii na management inayotakiwa hakuna ambacho hataweza kufanya. Mungu amjalie asidharau elimu ili aweze kutumia vizuri elimu yake kupata kila kinachostahili kutokana na kipaji chake.

Angalia Nishani ya Ufedhuli ya Lister Elia


Lister Elia ni mwanamuziki  Kitanzania aliyeko Japan. Hebu angalia upigaji wake wa Keyboards katika video hii. Vidole vikitembea kama mashine. Na hawa steji show wa Kijapani ni burudani nyingine tosha

IVORY BAND YAPANIA KUPAA KATIKA ANGA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA

Ijumaa hii na kila Ijumaa ni siku ya raha na starehe kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, maana mara tu baada ya jua kuzama kiota maaru...