Skip to main content

Posts

Showing posts from August 13, 2012

Historia ya muziki wa Tanzania

Historia fupi ya muziki wa Tanzania Kama ilivyokuwa kwa binadamu wengine, wakazi wa eneo ambalo hatimae limekuwa nchi yetu ya Tanzania, walikuwa na utamaduni wao. Utamaduni huu ulikuwa ukitofautiana kati ya kabila na kabila. Moja ya vipengele ilikuwa muziki. Kabla sijaendelea ni habari hii ni vizuri tukumbuke jambo moja, ikiwa kitu hakiko katika utamaduni wa kundi la watu, kitu hicho huwa hakina jina katika kundi lile. Nikiuliza unambie internet kwa kabila lako inaitwaje hutakuwa na jina hilo kwa kuwa hakuna kitu hicho katika utamaduni wa kabila lako. Hatukuwa na ‘muziki’ katika makabila yetu kabla ya ujio wa wageni, na hivyo hakuna kabila lenye tafsiri ya neno muziki. Lakini tuliimba, tulicheza ngoma, tulipiga vyombo mbalimbali, ila tulikuwa na utamaduni mwingine kuhusu kitu hiki tunachokiita siku hizi muziki. Watafiti wanatuambia tulikuwa na Ngoma, ambayo tafsiri yake ni kubwa kuliko muziki. Ngoma ilikuwa ni chombo kile kilichotoa muziki, ngoma ilikuwa shughuli yenyewe, kwa mfano ng…