Skip to main content

Posts

Showing posts from August 5, 2011

Sandton Sound, bendi yenye waimbaji ndugu

Sandton Sound bendi ambayo waimbaji wake ni wale ndugu Christian Sheggy na Francis Sheggy. Ni bendi nyingine ambayo haivumi lakini imo sana tu. Nimewakuta pale Legho Hotel Shekilango wakiporomosha muziki wa aina mbalimbali, ililazimika nishike gitaa pale walipoanza kuimba ule wimbo ambao ulikuwa utunzi wa Kyanga Songa ambao nilishiriki kupiga rythm gitaa miaka hiyo 1988/89. Masikitiko. Kwa wale wenye kumbukumbu kibwagizo chake kilikuwa Kinachonisikitisha ni kuona kwamba nakosa mume, Wakunioa mama, Nami nijisikie kama wenzangu waliobahatika kuolewa Hiyoooooo hiyoooo

Ras Nas- Nasibu Mwanukuzi mwanamuziki wetu aliyeko Norway

Nasibu Mwanukuzi maarufu kama  Ras Nas alizaliwa Morogoro, staili yake ya muziki ni kuchanganya muziki wa kiasili, reggae na kughani katika mfumo wa mashahiri. Ras Nas ni mwimbaji, mpiga gitaa, mshahiri, producer, na percussionist.  Nasibu alikuwa huku akisikia muziki wa miamba ya muziki ya Tanzania kama vile Mbaraka Mwinyshehe wa Morogoro Jazz, Wema Abdallah wa Western Jazz, Michael Enoch na gitaa lake enzi za Dar Jazz na wengine wengi waliokuwa wakipiga mitindo tofauti ya upigaji wa magitaa enzi hizo. Baadae akawasikiliza wanamuziki kama Bob Marley, Burning Spear, Gregory Isaac na hapo ndipo alipopata kujenga misingi ya muziki wake wa sasa. RaS Nas alipata digrii yake ya Uanasheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati akiwa hapo chuoni alianzisha kundi lililosheni wasanii wakali wa  Kuigiza na Ushahiri lililoitwa Sayari ambalo lilikuwa na wakongwe wengi kama Freddy Macha, Chiku Ali, Anna Lukindo,  George Chioko. Kundi hili lilichanganya muziki wa Kiasili, mashahiri, dansi na …