Ras Nas- Nasibu Mwanukuzi mwanamuziki wetu aliyeko Norway



Ras Nas

Ras Nas na Dekula Kahanga Vumbi katika tamasha la muziki la Mela
Nasibu Mwanukuzi maarufu kama  Ras Nas alizaliwa Morogoro, staili yake ya muziki ni kuchanganya muziki wa kiasili, reggae na kughani katika mfumo wa mashahiri. Ras Nas ni mwimbaji, mpiga gitaa, mshahiri, producer, na percussionist.  Nasibu alikuwa huku akisikia muziki wa miamba ya muziki ya Tanzania kama vile Mbaraka Mwinyshehe wa Morogoro Jazz, Wema Abdallah wa Western Jazz, Michael Enoch na gitaa lake enzi za Dar Jazz na wengine wengi waliokuwa wakipiga mitindo tofauti ya upigaji wa magitaa enzi hizo. Baadae akawasikiliza wanamuziki kama Bob Marley, Burning Spear, Gregory Isaac na hapo ndipo alipopata kujenga misingi ya muziki wake wa sasa. RaS Nas alipata digrii yake ya Uanasheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati akiwa hapo chuoni alianzisha kundi lililosheni wasanii wakali wa  Kuigiza na Ushahiri lililoitwa Sayari ambalo lilikuwa na wakongwe wengi kama Freddy Macha, Chiku Ali, Anna Lukindo,  George Chioko. Kundi hili lilichanganya muziki wa Kiasili, mashahiri, dansi na michezo ya kuigiza na kupata umaarufu mkubwa uliowezesha kundi hili kusafirikatika nchi mbalimbali za Scandinavia. Mwaka 1985 Nasibu alihamia Oslo Norway na amekuwa huko kuanzia hapo mpaka leo.  Ras anawatoto watatu.
 1990 Nasibu alianzisha alianzisha bendi yake aliyoiita RAS NAS. Mwaka 1997 akatoa album yake ya kwanza "Cut You Loose," July 2008 alitoa album nyingine Dar es Salaam.

Comments

Ras Nas said…
Asante Mkuu, tuko pamoja!!!
Ras Nas