Sunday, September 9, 2012

SINA MTOTO, ASEMA CHINEDU AKEDIEZE


Wiki chache zilizopita picha ya Chinedu, ilisambaa katika mitandao mbalimbali ikimuonyesha yuko na mtoto ambaye alitambulishwa kama mtoto wake. Lakini msanii huyu amekuja juu kuhusu picha hii na taarifa zilizoambatana nayo. 
Ametoa taarifa hii,’ Kila mtu anajua mke wangu ame graduate kutoka shule ya mitindo wiki chache zilizopita, je mlimuona ana dalili za mimba?. Ndio, picha hiyo ni yangu, ilipigwa 2008, nilikuwa nimemshika mtoto wa mmoja wa mashabiki wangu, kwa kweli sielewi nia ya aliyeanza kuisambaza picha hiyo kwa maelezo kuwa huyo ni mwanangu’

Mcheza sinema wa Kinaijeria atuhumiwa kumuuwa mkewe ni Rich Oganiru


Kwa wale wapenzi wa sinema za Kinaijeria jina au sura ya Rich Oganiru  si ngeni, ila wiki chache zilizopita alipata mkasa unaofanana sana na filamu zao. Baada ya kufiwa na mkewe na Oganiru alikamatwa kwa kosa la mauaji ya mkewe huyo, lakini kwa maelezo yake hadithi ni tofauti kabisa. Kadri ya maelezo ya Rich mkewe  aliaanza matatizo ya afya miezi mitano iliyopita akisumbuliwa na ‘fibroids’.Pamoja na mkewe kufanyiwa operesheni na daktari wa Kijerumani, fibroid hizo ziliendelea kukua na kumsumbua mkewe. Hivyo akajaribu kumpeleka mkewe kwa Prophet TB Joshua, wakati wanangoja kuonana nae mkewe alitoa wazo kuwa ahamie kwenye nyumba ya kaka yake kwenye kambi ya Jeshi la anga huko Shasha. Alipofika huko akawa anakataa chochote alicholetewa na mumewe na kuwa anakula kile tu alichopikiwa dada yake au kuletwana kaka yake. Hali yake ikaendelea kuwa mbaya, wakakubaliana kuhamia kwenye eneo la Sinagogi la TB Joshua kungoja appointment, lakini mkewe tena akabadili mawazo na kuomba kupelekwa hospitali ya Jeshi. Wakati wanampeleka wakiwa na shemeji yake, kaka wa mkewe huyo, mkewe alifariki wakiwa kwenye geti la hospitali. Rich alipoteza fahamu kutokana kupandwa kwa presha kwa kifo cha mkewe na kulazwa, alipozinduka, akakuta shemeji yake kishapeleka mwili mochwari lakini akamlazimisha yeye kwenda kuwaeleza wakwe zake kuwa binti yao kafariki. Aliomba apewe cheti cha kifo kusaidia kueleza kuhusu kifo hicho, lakini shemeji yake akawa mkali na kumfukuza toka hapo. Aliporudi kwenye hoteli ambako alikuwa akiishi akagundua kuwa kila kitu cha mkewe kilikuwa kimeondolewa chumbani na vitu vyake vimepekuliwa. Anasema hata funguo za gari lake na passport yake vilichukuliwa na akalazimika baadae kubembeleza shemeji yake amrudishie. Hatimae alipofika nyumbani kwake akakuta pia huko vitu vyote vya mkewe vimeondolewa mpaka picha zao za harusi. Baada ya siku tatu ndipo polisi walikuja kumweka chini ya ulinzi kwa mauaji ya mkewe. Alipofika rumande akakuta wafungwa walio wananchama wa Boko Haram wakawa wanamlazimisha kuwafulia nguo. Aliachiwa alipoonekana afya yake inadorora, lakini hata hivyo baada ya siku chache polisi walikuja tena na kumzoa tena kwa kipigo kikubwa. Rafiki yake ndie aliemsaidia kwa kulazimisha postmortem ifanywe kuona sababu za kifo ambapo baada ya kuonekana kilikuwa kifo kutokana na ugonjwa akaachiwa. Wakati akiwa kwenye hizi kasheshe, mke wake akazikwa bila taarifa kwake.....yaani stori kama filamu zao. Mungu amlaze pema mke wa msanii huyu

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD-YAPUNGUZA BEI

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
WAZEE WA KAZI
TUMESHUSHA BEI
NEW OFFERS TO MOMBASA/DAR
(from any port) 
4 X 4 CARS NOW          £780 
SALOON CARS NOW   £720 
PRICE DROP FOR CONTAINER SERVECES
40' TO MOMBASA/DAR £2,100
20' TO MOMBASA/DAR £1,350
WE CAN BEAT ANY QUOTE, JUST ASK!
KIFURUSHI KWA NDEGE £1.80
RATIBA YA MELI MPYA
Vessel: Asian Vision v117
Open for deliveries:  from:  5th September 2012
Ets: Tilbury: 23rd Sept 2012
Eta: Mombasa: 18th October
Eta: Dar Es Salaam 16th October
Vessel close:  21.00 /  19th September 2012

Asian Trust v099
Open for deliveries:  from 06.00 am/ 20th September 2012
Ets: Tilbury: 28th Sept 2012
Eta: Mombasa: 24th October
Eta: Dar Es Salaam 21st October
Vessel close:  21.00 / 26th September 2012
kama unataka kuagiza kitu au kufanya booking yoyote tutumie email au tupigie kwenye namba zifuatazo;

CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243
HASSAN (RICHARD) +44 07405159255
HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
 
Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

FFU ! NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA AFRIKA-MESSE,BREMEN


Bendi ya Ngoma Africa band aka FFU,
yenye maskani yake kule Ujerumani, inatarajiwa kutumbuiza katika maonyesho makubwa ya biashara ya kiafrika "AFRIKA-MESSE" Bremen,yatakayofanyika
mjini Bremen,Ujerumani. Ratiba katika maonyesho mawili yatakayofanyika wakati huo itakuwa kama ifuatavyo, Jumatano 12.09.2012 bendi itakua mjini Bremerhaven, na
Jumamosi ya 15.9.2012 Kikosi kazi hiko kitapeleka nguvu zote katika eneo la maonyesho