Wednesday, June 15, 2011

Birthday ya Babu Njenje ilishereheshwa na Cloud FM

Geah Habib


Babu Njenje

Dinah Marios


Babu Njenje na Bi Shakila


ZamaradyNdani ya studio za Clouds
Radio ya watu Clouds Fm imewezesha Birthday ya Babu Njenje kusherehekewa na maelfu ya watu nchini na nje ya nchi kwa kupitia radio na TV ya Clouds. Babu Njenje ametimiza miaka 64, hivyo Clouds iliweka hewani masaa matatu hewani kwa Bendi ya Kilimanjaro kuweza kushirikiana na Babu Njenje katika kusherehekea siku yake. Pamoja na Babu Njenje alikuweko ndani ya studio Bi Shakila, ambaye pamoja na kuwa walizaliwa mtaa mmoja na siku moja na Babu Njenje pia ililazimika Bi Shakila kwenda kunyonya ziwa la mama yake Babu Njenje kwa vile maziwa ya mama yake yalichelewa kutoka!!!!!!! Msanii mwingine aliyeimbiwa Happy Birthday ni Lady Jd ambaye nae leo ilikuwa Birthday yake. Pamoja na kuweko redioni Clouds waliweza kumuunganisha Babu Njenje kuzungumza na mkewe na wanae ambao kwa sasa wako nje ya nchi, Marekani na Uingereza. Bendi nzima ya Kilimanjaro ilikuweko na kuweza kuimba nyimbo mbalimbali za bendi katika studio.