Sunday, November 9, 2014

SIMON MWAKIFWAMBA APATA AJALI MOROGORO

Rais wa Shirikisho La Filamu Tanzania (TAFF), Mwakifwamba Simon, amepata ajali ya gari karibu na Mkundi, nje kidogo ya mji wa Morogoro karibu na mizani, usiku huu wakati akitoka Dodoma kuja Dar es Salaam. Gari aliyokuwa akiiendesha aina ya Toyota Noah T 176 CYM mali ya TAFF imepinduka na kuharibika vibaya, lakini yeye yuko salama. Kwa kadri ya maelezo ya Mwakifamba ni kuwa alipokata kona ghafla mbele akaona pikipiki ambayo haikuwa na taa wala reflector na katika kuikwepa na kuingia pembeni ya barabara tairi mbili zilipata pancha na gari kupinduka. Hakuna aliyeumia katika ajali hiyo. Mpaka tunapata taarifa hii alikuwa bado Morogoro akiandika maelezo kwenye kituo cha usalama barabarani.

KHAMIS AMIGOLAS KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KISUTU


RIP Amigolasy
KHAMIS AMIGOLAS  wanamuziki wa miaka mingi aliyepitia bendi kadhaa zikiwemo African Beat, African Stars na hatimae Ruvu Stars amefariki dunia jana usiku kutokana na ugonjwa wa moyo ambao wanaomfahamu wanasema ulikuwa ukimsumbua kwa miaka mingi. Khamis aliyefahamika sana kwa mustachi wake alikuwa mwanamuziki muimbaji mtulivu na mcheshi, mwenye kupenda utani sana.  Msiba uko jirani na shule ya Msingi ya Mianzini Mburahati. 
Mpaka sasa jamaa wa karibu wametaarifu kuwa mazishi yatakuwa kesho Jumatatu mchana katika makaburi ya Kisutu,
Mungu ailaze pema peponi roho yake Amin

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...