Rais wa Shirikisho La Filamu Tanzania (TAFF),
Mwakifwamba Simon, amepata ajali ya gari karibu na Mkundi, nje kidogo ya
mji wa Morogoro karibu na mizani, usiku huu wakati akitoka Dodoma kuja
Dar es Salaam. Gari aliyokuwa akiiendesha aina ya Toyota Noah T 176 CYM
mali ya TAFF imepinduka na kuharibika vibaya, lakini yeye yuko salama. Kwa kadri ya maelezo ya Mwakifamba ni kuwa alipokata kona ghafla mbele akaona pikipiki ambayo haikuwa na taa wala reflector na katika kuikwepa na kuingia pembeni ya barabara tairi mbili zilipata pancha na gari kupinduka. Hakuna aliyeumia katika ajali hiyo. Mpaka tunapata taarifa hii alikuwa bado Morogoro akiandika maelezo kwenye kituo cha usalama barabarani.
Comments