Skip to main content

Posts

Showing posts from August 29, 2012

JE TID ALIPANGA KUMUUA ALI KIBA?

Anga la muziki wa Tanzania limekumbwa na jinamizi jipya , ambapo mwanamuziki mmoja anadaiwa kupanga kumuua mwanamuziki mwingine.....kama ni kweli itakuwa ni hatua mpya kabisa katika anga za muziki kwa miaka mingi. Mara ya mwisho tasnia ya muziki kukumbwa na mambo ya mwanamuziki kuuwawa ni miaka ya sabini wakati mwanamuziki mmoja wa Orchestra Makassy alipokutwa kachinjwa katika bafu. Mungu apishe mbali. Haya ndio yanayozungumzwa katika mitandao mbalimbali leo hii.... Inasemekana meneja wa Ali Kiba amesema yafuatayo...... "Baada sasa ya taarifa hizo  kuifikia familia, iliamua kuripoti jambo hilo polisi, polisi walifika eneo lile na kulikuwa kuna watu wawili, mwanaume na mwanamke ambao walifika maeneo jirani na pale anapoishi Ali Kiba wakawa wameweka kambi pale kwa muda wakijaribu kupeleleza eneo lile.  Sasa baada ya watu wa karibu kuwaona na kutowatambua vizuri waliamua kuwafuatilia na kuwaweka chini baada ya kuwakamata. 
Walipowahoji vizuri wakasema kwamba ni kweli wao wame…