Anga la muziki wa Tanzania limekumbwa na jinamizi jipya , ambapo mwanamuziki mmoja anadaiwa kupanga kumuua mwanamuziki mwingine.....kama ni kweli itakuwa ni hatua mpya kabisa katika anga za muziki kwa miaka mingi. Mara ya mwisho tasnia ya muziki kukumbwa na mambo ya mwanamuziki kuuwawa ni miaka ya sabini wakati mwanamuziki mmoja wa Orchestra Makassy alipokutwa kachinjwa katika bafu. Mungu apishe mbali. Haya ndio yanayozungumzwa katika mitandao mbalimbali leo hii....
Inasemekana meneja wa Ali Kiba amesema yafuatayo......
"Baada sasa ya taarifa hizo
kuifikia familia, iliamua kuripoti jambo hilo polisi, polisi walifika eneo lile
na kulikuwa kuna watu wawili, mwanaume na mwanamke ambao walifika maeneo jirani
na pale anapoishi Ali Kiba wakawa wameweka kambi pale kwa muda wakijaribu
kupeleleza eneo lile.
Sasa baada ya watu wa karibu
kuwaona na kutowatambua vizuri waliamua kuwafuatilia na kuwaweka chini baada ya
kuwakamata.
Walipowahoji vizuri wakasema kwamba ni
kweli wao wametumwa kuja kufanya jambo hilo hapo kwa Ali Kiba na wao sio
wenyeji wa Dar es Salaam wametoka mikoani. Walipoulizwa ni nani ambaye
amewatuma kuja kufanya hilo jambo wakawa wamemtaja TID Kwamba moja kwa moja
yeye ndio anahusika.
Basi moja kwa moja gari la jeshi la
polisi likaenda kumkamata TID na hatimaye kumfikisha kwenye kituo cha polisi
cha kati ambapo yupo mpaka hivi sasa anashikiliwa."
Ameongeza kuwa TID na watu hao walikutana katika maeneo ya Mtoni Kijichi
kupanga mpango huo wa kumuua Ali Kiba....TID mwenyewe alikuwa na haya yakusema......
Alipohojiwa na Soudy
Brown, T.I.D amesema “kwa nini nimuue Ally Kiba bwana, si mtu wangu nampenda
kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari,
nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo,
kwa sababu gani? toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha
muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi,nia ya hao watu ni
kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe”
Comments