Thursday, October 18, 2012

RayC - Rehema Chalamila

Rehema Chalamila binti mwanamuziki maarufu aliyezaliwa Mafinga, Iringa  May 15, 1982 maarufu kwa jina la  Ray C na pia kwa kiuno bila mfupa, ambae ameweza kufurahisha nyoyo za wengi kwa sauti yake tamu, kwa wakati huu inasemekana yuko katika mtihani mkubwa wa kujaribu kuacha kutumia madawa ya kulevya. Kumekuweko hadithi mbalimbali kwa muda mrefu kuwa anajihusisha na matumizi ya madawa hayo, hatimae sasa inadaiwa hali imefikia pabaya kiasi cha kulazimika kuingia kwenye hospitali zenye utaalamu wa kusaidia kuacha matumizi ya madawa hayo(Rehab). Ikiwa ni kweli wote tuliokuwa tukipenda muziki wake tumuombee Mungu ampe nguvu aweze kushinda mtihani huu mgumu

LADY HANIFA KAZINI

Lady Hanifa

Lady Hanifa na Suba Mkole

Mzee Manyema (kulia)

Katika pita pita yangu nimemkuta mtangazaji maarufu wa ITV Lady Hanifa akiwa kazini akiwahoji wanamuziki kutoka vipindi viwili mbalimbali. Alianza kwa kufanya mahojiano na mwanamuziki muimbaji wa siku nyingi Mzee Manyema (Sokolokwinyo) na hatimae akawahoji wanamuziki wa kizazi cha sasa wanaojiita Suba Mkole.

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...