Friday, March 16, 2012

Rais wa Shirikisho la Filamu(TAFF), Simon Mwakifwamba afiwa na mwanae

Katika mazishi yaliyotia majonzi makubwa Bwana Simon Mwakifwamba leo amemzika mwanae Benjamin ambae alikuwa na umri mdogo wa miaka mitano tu. Pole sana Simon na Mama Benjamin. Mungu alitoa na Mungu ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe

Benny Omar na Abou Omary wafiwa na baba yao

Ben Omary

Abuu Omary
Wanamuziki waliopo juu kama ilivyokuwa imeelezwa awali katika blog hii wamefiwa na baba yao mzazi Mzee Omar Abubakar Njenga,baada ya kuugua tangu mwishoni mwa mwaka jana(2011). Kifo kimetokea katika hospitali ya Lugalo na mipango ya kuusafirisha mwili kwenda Nachingwea kwa mazishi inafanywa nyumbani kwake Mbagala.
Mzee Njenga alikuwa mfanya kazi wa Agip (T)Ltd(enzi hizo), hadi alipostaafu 1992,alikuwa kikazi zaidi makao makuu mtaa wa Msimbazi/Mkunguni pia aliwahi kushi Moshi na Iringa kikazi.Mungu Amlaze Pema Mzee Njenga Amin

IVORY BAND YAPANIA KUPAA KATIKA ANGA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA

Ijumaa hii na kila Ijumaa ni siku ya raha na starehe kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, maana mara tu baada ya jua kuzama kiota maaru...