Skip to main content

Posts

Showing posts from November 27, 2011

Anti virus na Str8t Muziki ukurasa mpya katika music industry

Jana tarehe 26 November 2011 kulifanyika maonesho mawili makubwa ya muziki. Str8t Muzik Inter-College Festival 2011 na lilioitwa Tamasha la Anti Virus. Maelfu ya watu, walikusanyika katika viwanja vya Leaders na viwanja vya Ustawi wa jamii. Kuna watu walitoka hata nchi za jirani kuja kuhudhuria shughuli hizi. Siku hii itakumbukwa pia katika uwingi wa watu waliohudhuria katika show za muziki. Str8t Muziki pamoja na kuwa na wasanii wanachi ilikuwa pia na wasanii kutoka nje Faboulous na DMX, japo DMX hakutokea, kuna maelezo tata kwa nini hakutokea. Tamasha la Anti Virus lilikuwa ni la wasanii wazalendo na wengi ambao wamesha wahi kuwa majina makubwa nchini, na wengine kutosikika kwa muda mrefu, lakini ni wazi umati wa watu ulionyesha kuwa pamoja na vyombo vya utangazaji kuwafuta katika anga zao bado wamo kwenye mioyo ya watu wengi uwingi wa watu katika tamasha hili lililokosa udhamini ni ushahidi tosha wa kisayansi kwa hilo. Kufanikiwa kwa matamasha makubwa yenye watu wengi kwa wakati mmo…