Monday, October 17, 2011

Kilimanjaro Band wakiwa kazini na wimbo wao wa Gere

Kati ya nyimbo nyingi ambazo zimependwa za Kilimanjaro Band ni huu wimbo wa Gere ambao asili yake ni katika upande wa Magharibi wa Nchi yetu ya Tanzania. Bi Nyota ambaye sauti yake ni kati ya sauti tamu za waimbaji wa kike akiwa anaimba wimbo huu Diamond Jubilee.

Tanzania Moto Modern Taarab kuzinduliwa Oktoba 28

 Bendi Kongwe nchini, Msondo Ngoma na bendi inayokuja juu katika wigo wa muziki wa dansi Mapacha Watatu watakuwa pamoja na kundi jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarabb (T-Moto) ‘Real Madrid’ katika uzinduzi wa kundi hilo utakaofanyika Oktoba 28,2011 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mkurugenzi wa kundi hilo la Tanzania Modern Taarab, Amini Salmini, alisema kuwa  uzinduzi wa kundi hilo utafanyika sambamba na uzinduzi wa albam yao kwanza ya inayokwenda kwa jina la Aliyeniumba Hajanikosea.

Listening Party ya album ya 11 ya Twanga Pepeta...usikoseee

Tujumuike wote kwenyeListening Party ya Albam ya 11 ya The African Stars Band wana Twanga Pepeta " DUNIA DARAJA" kesho Jumanne MAISHA CLUB, kuanzia  saa 2 usiku. Bendi yenye uzoefu wa kutoa burudani miaka kemkem.