Skip to main content

Posts

Showing posts from September 1, 2011

Papa zi kuwa mdhamini mwenza katika Vodacom Miss Tanzania 2011

Mkurugenzi wa Papa Zi Arts and Entertaiment, Zachary Hans Pope ametangaza udhamini wa kampuni yake katika shindano la Vodacom Miss Tanzania. Akiwa na Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga, Mkurugenzi huyo alitangaza kuwa kampuni yake itadhamini warembo watatu watakaopenda kujiingiza katika Ulimwengu wa sanaa za maigizo katika filamu, pia atakaye kuwa Miss Papazi atapata US$ 1000, Bwana Pope alisema kuwa Papazi pia itaongeza zawadi kwa washindi wa tatu wa mwanzo wa Vodacom Miss Tanzania


Sinza Sound Band

Sinza Sound Band ni 'resident band' ya Johannesburg Hotel iliyoko Sinza Mori. Kila Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, bendi hii huporomosha muziki kwa ajili ya wageni wanaotembelea hotelini hapa. Bendi hii hupiga muziki wa aina mbalimbali, nilipata bahati ya kukaribishwa kwa wimbo wa Ngalula(Maquis Original), Masafa Marefu(Tancut Almasi),Christina Bundala(DDC Mlimani Park), Nakupenda Cherie(Simba wa Nyika) nikabaki napata raha ya nyimbo nyingi nilizozipenda.