Sunday, April 17, 2011

FM Academia, New Msasani Club

Nyoshi el Saadat na Mwamba ambae pia ni msanii muigizaji wa filamuKila Jumapili kuanzia kumi na mbili jioni, New Msasani Club huwa panatawaliwa na muziki mzito wa FM Academia. Nyoshi akiwa analiongoza kundi zima huleta burudani tosha ya kuimba na kucheza bila kuchoka na kwa kweli ni raha tupu. Nimekutana na dada mmoja ambaye kwa usiemjua utadhani bado ni msichana mdogona alikuwepo hapo na wanamuziki wa FM, huyu namkumbuka aliwahi kuwa na ukaribu huo huo na wanamuziki wa TANCUT , baadae nikamkuta na wanamuziki wa Vijana Jazz miaka hiyo mwishoni mwa themanini, leo nimemkuta na wanamuziki wa FM Academia kweli huyu ni mpenzi wa muziki

Simon na sequencer Kalabash Bar Mwenge


Simon
Rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kunambia njoo hapa Calabash Mwenge ufaidi, kuna bendi inapiga nyimbo za bendi ya Tancut. Nilipowasili toka nje nikasikia kibao cha zamani cha DDC Mlimani park, nikajiuliza nani hawa. Nilipoingia nikamkuta rafiki yangu Simon na mwenzie. Simon akiwa kwenye keyboards na mwenzie guitar, na wote wakiimba huku vyombo vikipiga kwa mtindo wa sequencer. Walikuwa wanapiga vizuri sana. Nikakumbuka mbali sana. Nikamkumbuka Simon alipokuwa mdogo, mwanzoni mwa miaka ya 90, akawa anakuja Vijana Jazz enzi za Vijana Day na kuingia katika mashindano ya kuimba tuliyokuwa tunayawafanya wakati huo. Watoto kwa wakubwa walikuwa wakishindana kuimba nyimbo za Vijana na mshindi kupewa zawadi mbalimbali, kama radio, ndoo, kanga sahani saa za ukutani na kadhalika. Simon alikuwa akishinda mara kwa mara, kwa sasa ni mwanamuziki wa hali ya juu ambae amekwishafanya ziara nyingi nchi za nje. Juma Katundu wa Msondo nae ni zao la mashindano hayo

Bonanza Leaders Club

Kila Jumapili mchana kunakuweko na kitu kinaitwa Bonanza pale Leaders Club. Bendi ya African Stars International, maarufu kama Twanga Pepeta ndo huwa inatumbuiza hapo kama kawaida huwepo wao na wapenzi wengine mbalimbali wa muziki

MCD
Twanga kwa nyuma

Victor Mkambi

Shakashia na Luiza

Kimobitel kamoon

Zungu mcheza show wa Twanga amabaye ni mtoto wa mmoja wa wanamuziki wapiga gitaa wa Afro70. Salim Willis

Kocha wa Dunia

Rapaaaaaaaaaaaa

Mshindi wa Singeli Michano ya EFM Mwanza apatikana

> Watanzania jana waliadhimisha kumbukizi ya miaka 18 tangu kufariki dunia kwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl.Julius Kambara...